21 WAOKOLEWA WENGINE HAWAJULIKANI WALIKO BAADA YA JAHAZI KUZAMA, Likitoka Tanga kwenda Zanzibar na abiria 32. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, January 31, 2013

21 WAOKOLEWA WENGINE HAWAJULIKANI WALIKO BAADA YA JAHAZI KUZAMA, Likitoka Tanga kwenda Zanzibar na abiria 32.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji abiria wa Jahazi ya Sun Rise Juma Ali Jaku, iliyopata ajali na kuzama  kati ya Tanga na Mkokotoni ikiwa imebeba Abiria 32 kati ya hao 21 wameokolewa na saba hadi sasa hawajapatikana katikati ni Mkewe balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis.
Nahodha wa Jahazi ya Sun Rise  iliyozama kati ya Tanga na Mkokotoni Bwana Abdulla Saleh akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mkasa uliowapata wa kuzama baada ya chombo chao kupatwa na dhoruba kali.
WATU 11 wakiwemo watoto watatu hawajulikani waliko baada ya Jahazi walilokuwa wakisafiria kutoka Tanga kwenda Zanzibar kupata dhoruba na kuzama karibu na visiwa vya Zanzibar majira ya saa 11 za alfajiri leo.
Akizungumza kutoka Hospitali ya Kaskazini A Kivunge nahodha wa Jahazi hilo Abdullah Saleh, ambaye amenusurika alisema jahazi hilo lilikuwa limepakia abiria 32, lakini lina uwezo wa kupakia abiria 50.
Alifafanua kuwa safari yao ilianzia Tanga majira ya Saa nane za Usiku lakini hali ya hewa ilibadilika ghafla majira ya saa 11 alfajiri na kusababisha Chombo hicho kuzama.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa Zanzibar amewapa pole abiria waliokolewa baada ya kuwatembelea hospitalini hapo ambapo pia alimpongeza nahodha wa chombo hicho kutokana na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la kuokoa abiria waliozama kwenye chombo hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here