TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa
saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y.
Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa
2013.
Mheshimiwa
Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha,
Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wa Tanzania.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete
amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha
kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini. Taarifa iliyotolewa mjini
Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue,
leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya
Januari 22, mwaka huu, 2013.
Aidha,
taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha
kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini.
Taarifa
iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza
Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013. Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla
ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji.
Imetolewa
na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013
|
No comments:
Post a Comment