Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Addo Mapunda (kushoto) akibadilishana mkataba na mratibu wa mpango huo Bi Anne Devilliers. Mpango huo utazinufaisha shule mbalimbali za sekondari wilayani humo.
WANAFUNZI wapatao 1580
wa shule tisa za sekondari Wilayani Kilwa Mkoani Lindi wanatarajiwa kunufaika
na mpango wa elimu wa mafunzo ya lugha ya Kingereza kwa njia ya Technolojia ya
kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni inayojihusisha na uchimbaji,
usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.
Mradi huo wa miaka mitatu
unatarajiwa kugharimu kiasi cha Tsh.144,945,218. Zitakazotumika kujenga misingi
bora ya lugha ya kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia mwaka
2013.
Hayo yameelezwa na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Adoh Mapunda wakati akitoa taarifa
kwenye hafla fupi ya utiaji saini wa mpango huo.
Mafunzo hayo yaliyoanza hivi karibuni
yanatolewa na walimu wapatao 30, wakiwemo wakigeni 12(Volunteeers) na wazawa
18, ambapo kwakuanzia yanatarajiwa kufanyika kwa wiki 6.
Kwenye Shule hizo tisa
kila moja italazimika kutoa walimu wawili ambao watapatiwa mafunzo kwaajili ya
kuendeleza mpango huo katika shule zote.
Mkurugenzi huyo alizitaja
shule zitakazonufaika na mpango huo ni, Kilwa day iliyopo mji mdogo wa Kilwa
masoko, Mtanga, Songosongo, Mbuyuni,Kinjumbi, Miteja, Mingumbi, Kikanda na
Sekondari ya wasichana Ilulu.
|
No comments:
Post a Comment