![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxsLgekrRXB2XOxVXTwgTG4e3kZUGa6ArSIlw9PLWA6BtkdJeDQMJxPB4k3gus1X21f7vz7S4BsOXODB2TkJvkfgIeT6rmcvSbvtSSLeDvR9j9jDAwfEFIp83Umr-b6g9MlsQmhK8w2BV1/s640/kkkkk.jpg)
Taarifa kutoka afisi ya rais
zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu
usiku.
Taarifa
zinazohusiana
Msaidizi wake pia amethibitisha
kufariki kwa kiongozi huyo.Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji
wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais. Rais Attah
Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda
mfupi baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo
alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa
afya yake. Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama
anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda
katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa
ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.Wakati wa uongozi wake, uchumi wa
Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi." Ni kwa masikitiko makuu na
kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana
" taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills
mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.Hata
hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.Lakini msaidizi wake mmoja ambaye
hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya
Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae
kufariki mapema siku ya Jumanne.Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa
mafuta nchi Ghana.
No comments:
Post a Comment