Na
Mwandishi Wetu
MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pop ametoa msaada wa dola
1000
(zaidi ya Sh milioni 1.5) kwa beki wa zamani wa timu hiyo, Alphonce
Modest
anayesumbuliwa na maradhi ya ganzi.
![]() |
| Zacharia Hans Poppe. |
Modest
yuko jijini Dar es Salaam akiendelea na matatibu chini ya usimamizi wa
gazeti
la Championi kwa kushirikiana na kipindi cha michezo cha radio ya Magic
FM.
Akizungumza
na Championi Ijumaa, Mtangazaji wa Magic FM, Said Kilumanga ambaye ni
mmoja wa
waratibu wa zoezi hilo alisema tayari Hans Pop ameshakabidhi fedha hizo.
“Tunamshukuru
sana Hans Pop kwa moyo wa
kujitolea, wengine pia wajitokeze kumsaidia kwa kuwa amepungukiwa kama
Sh
600,000 tu ili kukamilisha matibabu yake,” alisema Kilumanga.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion, Alex Msama ndiye alikuwa mdau wa kwanza kumchangia
Modest
na kuomba wengine wajitokeze kumsaidia beki huyo mahiri wa zamani.
Baadhi ya
wanamichezo wamekuwa wakiendelea kumchangia Modest ili kuhakikisha
anapata
matibabu baada ya maradhi hayo kumuandama kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Kwa wengine
walio tayari kumsaidia, wanaweza kuwasiliana au kutuma michango yao
kupitia
namba zifuatazo 0718427426
narudia tena 0718427426.


No comments:
Post a Comment