Maandamano ya kuipinga
Japani yameendelea katika miji kadha ya Uchina katika mzozo unaozidi kuhusu
visiwa vilioko katika bahari ya kusini ya Uchina.
Waandamanaji wakikwepa mabomu ya machozi nchini China nje ya Ubalozi wa Japan kuipinga nchi hiyo ya Japan kuhodhi visiwa vilivyopo bahari ya kusini mwa China.Polisi wakikabiliana na waandamanaji.
POLISI walitumia gesi kutawanya watu waliokuwa na hasira
kwenye mji wa Shenzhen, kusini mwa Uchina, huku waandamanaji wakichoma bendera
za Japani katika mji wa jirani, Guangzhou.
Japan imetoa wito kwa Uchina kuhakikisha usalama wa raia wa
Japani, huku Uchina imezidi kusisitiza madai yake ya visiwa hivo viitwavyo
Senkaku au Diaoyu. Kwa miaka mingi hayakutokea maandamano ya ghasia Uchina kama
haya, kuipinga Japani.
Watu waliokuwa na hasira walichoma moto bendera ya Japani,
walibeba mabiramu ya kuitusi Japani na kurusha mawe ubalozini.Karakana na
biashara za Japani piya zililengwa na waporaji na kuchomwa moto. Hata hivo
maandamano hayo hayakutajwa na vyombo vya habari vya taifa na juhudi zimefanywa
kudhibiti majadiliano kwenye internet.
Sababu ni kuwa maandamano yenyewe ni mazuri kufikisha ujumbe
kwa Japani, lakini yanaweza kugeuka na kuwa dhidi ya serikali piya. Wakuu wa
Uchina wanaamini kuwa Japani imevunja makubaliano ya namna fulani, kwamba hali
ibaki kama ilivokuwa.
Serikali ya Japani inasema inavinunua visiwa hivo kutoka
serikali ya mji wa Tokyo ili kuzuwia serikali ya jiji kufanya miradi na kujenga
katika visiwa hivyo. Lakini Uchina inaona hatua hiyo ni juhudi za kuthibitisha
kuwa visiwa hivyo ni vya Japani.
No comments:
Post a Comment