Na Abdulaziz
Video, Kilwa Masoko
Wakati zikiwa zimebaki siku chache kufikiwa na Tume ya Ukusanyaji wa Maoni ya Mchakato wa Katiba mpya inayoendelea Mkoani Lindi, Wananchi wa Wilayani Kilwa Wameombwa kuhudhuria katika mdahalo wa Uhamasishaji na kujenga uelewa juu ya Utoaji wa Maoni Yao
Mdahalo huo Utakaofanyika katika Ukumbi wa
Jumba la Maendeleo Wilayani Humo ambao umeandaliwa na Mtandao wa Asasi zisizo
za kiserikali wilayani Kilwa na Kufadhiliwa na The Foundation for civil
society ni harakati za kuongeza ushiriki wa Jamii ikiwemo
wa Vyama vya siasa,Taasisi za Dini, Halmashauri ,Wazee wakiwemo vijana katika mchakato wa kupata katiba mpya
TANZANIA
Asasi ya Kingonet itafanya mdahalo kesho Jumatatu tarehe 10 na kuanza saa 3 asubuhi
Wakati zikiwa zimebaki siku chache kufikiwa na Tume ya Ukusanyaji wa Maoni ya Mchakato wa Katiba mpya inayoendelea Mkoani Lindi, Wananchi wa Wilayani Kilwa Wameombwa kuhudhuria katika mdahalo wa Uhamasishaji na kujenga uelewa juu ya Utoaji wa Maoni Yao
![]() |
| Omary Mkuwili kushoto. |
Asasi ya Kingonet itafanya mdahalo kesho Jumatatu tarehe 10 na kuanza saa 3 asubuhi
Akizungumza
na blogu hii, Katibu wa Kingonet, Bw Omary Mkuwili alieleza kuwa Asasi yake ina
lengo la kuwajengea Uelewa ili Jamii wilayani humo kutumia Fursa hiyo kushiriki
kwa ukamilifu na kutoa maoni yatakayosaidia jamii kuishi na kufuata katiba
ambayo itakuwa ya kwanza kutungwa na Watanzania wenyewe kufuatia maoni yao
watakayoyatoa
‘’Nawaomba
wana Kilwa kutumia fursa hii na kujitokeza kwa wingi kesho ili kupata fursa ya
kuelewa na kujengewa uwezo wa jinsi ya kutoa maoni yao kabla Tume haijafika
wilayani Kilwa hii ni fursa pekee iliyotolewa na Kingonet kupitia The Foundation
Ni nafasi adimu Tuitumie kwa Maendeleo ya Kilwa na Tanzania…..Alimalizia
Mkuwili
Tume ya
Maoni ya Katiba ikiongozwa na Mama Salama Kombo Ahmeid ipo Mkoani Lindi tangu
August 28,2012 ambapo ilianza katika wilaya ya Liwale,Nachingwea na sasa wapo
katika Wilaya Ruangwa
Kwa Wilaya
ya Kilwa Tume hiyo itaanza kazi zake tarehe 24 ya mwezi huu.

No comments:
Post a Comment