![]() |
Polisi Jijini Nairobi wakipekua mabaki ya vifaa vya shule vilivyolipuliwa na guruneti leo asubuhi ambapo mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye shule ya Saint Polycarp.
|
![]() |
Askari wa Kenya wakiangalia eneo ambalo guruneti lillipita kwenye
shule hiyo.
|
Shambulio la guruneti la mkononi dhidi
ya shule ya Jumapili ya watoto wa Kikristo mjini Nairobi limeuwa mtoto mmoja na
kujeruhi wengine kadha.
Mkuu wa polisi wa Nairobi, Moses
Ombati, ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba watu watatu wamekamatwa, na
kwamba watu hao walionekana wakipiga picha za kanisa la Saint Polycarp
lilolengwa.
Msikiti ulio karibu na hapo
ulishambuliwa na vijana waliokuwa na hasira.Afisa wa polisi wa Nairobi
aliwasihi watu wawe watulivu. Shambulio lilitokea katika mtaa wa Juja Road,
unaopakana na mtaa wa Eastleaigh.
Inaaminiwa kuwa guruneti lilirushiwa
kanisa la Saint Polycap kama saa tano punde baada ya misa ya asubuhi.
Kundi lilokuwa na hasira
limewashambulia Wasomali katika mtaa wa Eastleigh, Nairobi, baada ya
guruneti kurushwa kwenye shule ya Jumapili ya watoto wa Kikristo, na
kuuwa mtoto mmoja na kuwajeruhi kadha.
Polisi waliwatawanya vijana ambao waliwalenga
Wasomali wa mtaa wa Eastleigh. Polisi wanasema watu 13 walijeruhiwa katika
mashambulio hayo ya kulipiza kisasi. Katika mashambulio ya karibuni dhidi ya makanisa nchini Kenya, wamelaumiwa wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab wa
Somalia, ambako wanajeshi wa Kenya wakishirikiana na wale wa Umoja wa
Afrika wanapambana na wapiganaji hao.



No comments:
Post a Comment