![]() |
| Kamanda Kenyela. |
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam , Mratibu wa pambano hilo linalosimamiwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Regina Gwae, alisema mbali Kamanda Kenyela, kutakuwa na wageni wengine maalum akiwemo Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan.
Alisema wanashukuru kwa ushirikiano wa viongozi hao katika maandalizi na hatimaye wamethibitisha ushiriki wao katika pambano hilo ambalo linavuta hisia za watu wengi na wapenzi wa ngumi jijini Dar es Salaam.
Alitaja mapambano manne ya utangulizi ya siku hiyo ambapo Abdul Awilo atazichapa na Shedrack Juma, Selemani Shaaban atavaana na Hamisi Mohamed huku Jonas Segu akinyukana na Ibrahim Class wakati Charles Mashali atatwangana na Teacher Aaron.
“Tumeamua kuchukua mabondia kutoka katika klabu zenye mashabiki wengi, tumechukua kwa Mzazi tumechukua klabu ya manzese anakotoka Mashali na Super D Boxing Club,’ alisema Regina.
Regina alisema, bondia Medi Sebyala na Kocha wake wanatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 11 na tayari maandalizi ya safari yao yamekamilika, ikiwemo kuwatumia tiketi na wameshazipokea.


No comments:
Post a Comment