REDDS MISS TANZANIA WAMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU NYUMBANI KWAKE. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, October 10, 2012

REDDS MISS TANZANIA WAMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU NYUMBANI KWAKE.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, akizungumza na Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 waliofika nyumbani kwake Monduli leo na kupata wasaa kwa kuzungumza nae mambo mawili matatu juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa  kwa ujumla.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Msimamizi (Matron) wa warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012, Irene Karugaba wakati Warembo hao walipotembelea Nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Monduli ili Kupata Baraka zake.Mh. Lowassa aliwapokea warembo hao kwa furaha na kuzungumza nao machache juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here