Mwanamke ambaye jinalake halikuweza kufahamika maramoja akiwa amelala chini baada ya bodaboda aliyokuwa amepanda kugongwa na greda lakuchonga barabara kwenye ajali
mbaya iliyohusisha Greda na Bodaboda. Ajali hiyo imetokea alasiri hii mjini Musoma
kwenye makutano ya Barabara ya Shabani na Bus Stop. Ajali hiyo
imepelekea abiria aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki hiyo kujeruhiwa
vibaya maeneo ya tumbo baada ya kuburutwa na mashine hiyo ya
kutengenezea barabara. Hata hivyo limetokea gari la shirika la umeme
Tanesco na kumchukua majeruhi huyo na kumkimbiza katika hospitali ya
Mkoa wa Mara. Mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tuio kulikuwa na
sintofahamu ya ni wapi dereva wa pikipiki na greda hilo walipoelekea
kwani mashuhuda wa tukio hilo wanasema dereva wa pikipiki alikimbia
punde tu ajali ilipotokea.
Pikipiki iliyohusika kwenye ajali hiyo!
Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo!Picha kwa hisani ya Mara yetu.
No comments:
Post a Comment