KINA MAMA KIPAWA WAPATIWA MAFUNZO YA WAJASIRIAM​ALI. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, December 17, 2012

KINA MAMA KIPAWA WAPATIWA MAFUNZO YA WAJASIRIAM​ALI.

Naibu Waziri wa Ajira na Kazi na Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga akitoa neno fupi wakati akifungua semina ya wajasiriamali wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala. Semina hiyo ni ya siku moja ni ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika ukumbi wa Air Wing Dar es Salaam leo. Semina hiyo ilifadhiliwa na Benki ya Equity na Darling Hair kwa msaada wa Diwani wa Kata hiyo Bonnal Kaluwa (kulia).

Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga kufungua mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali wa Kata ya Kiapawa leo asubuhi.

Wakina mama wajasiriamali wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala wakifuatilia semina yao ya siku moja ya mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika ukumbi wa Air Wing Dar es Salaam jana. Semina hiyo ilifadhiliwa na Benki ya Equity na Darling Hair kwa msaada wa Diwani wa Kata hiyo Bonnal Kaluwa.
Akina mama hao wakifuatilia mafunzo.
             

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here