TANESCO KUTUMIA BILION 40 KUFUNGA UMEME MAJUMBANI. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, December 24, 2012

TANESCO KUTUMIA BILION 40 KUFUNGA UMEME MAJUMBANI.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme wakati wa sikukuu za mwisho wa  mwaka. Kulia ni mmoja wa maofisa  habari wa shirika hilo, Nyasigo Emanuel.
 Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), litatumia sh. bilioni 40 kwa ajili ya kubeba gharama za ufungaji wa umeme kwa wananchi 250,000 kwa mwaka baada ya kupunguza gharama hizo.

Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu hali ya upatikanaji umeme nchini wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Mramba alisema hali hiyo itampunguzia mzigo mwananchi ambapo sasa gharama kubwa za ufungaji wa umeme katika majumba zitabebwa na shirika hilo.

"Katika kufanikisha suala hili Serikali nayo itachangia kiasi fulani cha gharama katika uingizaji wa umeme huo katika majumba lengo likiwa ni kutoka asilimia 18 na 20 tulizopo na kufikia asilimia 30 kama Rais Jakaya Kikwete alivyopendekeza," alisema Mramba.

Alisema bei mpya za umeme zitaanza kutumika kuanzia Januari mwakani na kuendelea na kuwa shirika hilo hivi sasa linaunganisha umeme kwa mteja aliyeomba katika kipindi cha wiki moja ambapo zamani ilikuwa ni miezi sita. Mramba alisema zamani shirika hilo lilikuwa likiwafungia umeme wateja 20,000 hadi 25,000 kwa mwaka, lakini hivi sasa wamepiga hatua ambapo idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia wateja 80,000 hadi 100,000.

Aliongeza kuwa katika ushindani wa kufanyakazi katika ofisi zingine za mikoani wamepanga kumwekea mteja atakayekwenda kipindi cha sikukuu kuomba kufungiwa umeme na atawekewa kwa siku moja tangu aombe. Mramba alisema tatizo la kukosekana kwa umeme wa uhakikia litakwisha kipindi kifupi kijacho kwa vile miradi mingi ya kujenga miundombinu inaendelea ikiwa ni pamoja na ubadilishaji wa transifoma mpya kote nchini.


Alisema shirika hilo limejipanga kuhakikisha katika kipindi cha sikukuu umeme wa uhakika unapatikana na kuwa mafundi wao watakuwepo katika vituo vyao vya dharura kwa saa 24. Mramba alitumia fursa hiyo kuwaondoa hofu Watanzania kwa kuwaeleza kuwa hivi sasa hali ya umeme nchini imeimarika na kukatika kwa umeme kunakotokea ni matatitizo ya kawaida na si mgawo kama inavyodaiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here