MSANII
maarufu nchini, Elizabeth Michael (Lulu), anayekabiliwa na mashitaka ya
kumuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba, amedai mahakamani
kwamba walikuwa wapenzi, walipendana sana lakini hawakuaminiana.
“Siku
mbili kabla ya kifo chake alitabiri kifo hicho kwani alinitumia ujumbe
unaosema, nitakufa kwa ajili yako, nakupenda sana,” hayo yalikuwa maneno
ya Lulu aliyoyatoa Polisi wakati akihojiwa.
Muhtasari huo wa
ushahidi ulisomwa jana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka
mbele ya Hakimu Mkazi Augustino Mmbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Kweka alidai, Sajenti Revonatus aliyechukua maelezo ya
Lulu baada ya tukio, alidai lulu alianza uhusiano wa mapenzi na Kanumba
Junuari mwaka huu, katika uhusiano wao walikuwa wanagombana kama mtu
atapokea simu ya mwenzake.
Alidai Lulu wakati akiwa Mikocheni kwa
rafiki yake Ritha, kabla ya kutoka akampigia simu mpenzi wake Kanumba
na kumwambia kuwa anataka kutoka, alipofika nyumbani kwa Kanumba
alimkuta anazungumza na simu.
Lulu alidai na yeye alipigiwa simu
na rafiki yake wa kike, alipotaka kwenda kupokea simu nje Kanumba
alimzuia asitoke nje na yeye alitoka nje na ndipo Kanumba alipomkimbiza
mpaka barabarani.
Alipomshika akaanza kumpiga makofi na mateke,
walipoingia ndani, Kanumba alimtupa kitandani na kuchukua panga chini ya
kitanda kisha kuanza kumpiga na ubapa wa panga katika mapaja yake.
“Lulu
alikubali kutoa maelezo hayo akiwa peke yake na kwamba alikuwa huru
katika uhusiano wake na Kanumba, kwani alikuwa anaenda kulala kwake kila
alipokuwa akijisikia kufanya hivyo, lakini hawakuwahi kuishi pamoja.
“Aprili
5 mwaka huu usiku, Kanumba alimtumia ujumbe kuwa ‘you will kill me soo,
I love you so much, akamfariji kwa kumwambia kuwa achana na mambo hayo
na akawa sawa.
“Tarehe 6, Kanumba alimpigia simu na kumwambia
anatarajia kusafiri kwenda Marekani April 14, mwaka huu amletee zawadi
gani naye akamjibu zawadi yoyote,” alidai Kweka wakati akisoma muhtasari
wa ushahidi.
Alidai walikuwa wanapendana lakini hawaaminiani
wakiwa mbali, kwani Kanumba alikuwa na wivu wa kimapenzi na alikuwa
anasema anamdharau.
Mshitakiwa alidai hakumsukuma Kanumba,
Kanumba alivyompiga na ubapa wa panga alilitupa chini na kuanza kuhema
kwa hasira ambazo hakuwahi kuona tangu wawe wapenzi.
Alidai
mshitakiwa alijigonga kisogoni katika ukuta na kuanguka chini, lakini
alipomuona kama anataka kunyanyuka, alikimbilia chooni na kujifungia
ndani, baada ya muda aliona Kanumba anatokwa na povu ndipo alimwagia
maji na kutoka nje kwenda kumwita mdogo wake Seth.
Lulu alipopewa nafasi ya kusema chochote katika Mahakama ya Kisutu, alisema hana chochote cha kusema.
“Nawatakia
mafanikio mema huko Mahakama Kuu katika kesi hii, nawashukuru mawakili
wote, waandishi wa habari na wananchi wote ambao tumeshirikiana pamoja,
Lulu utarudi gerezani mpaka utakapoitwa Mahakama Kuu,” alisema Hakimu
Mmbando.
Upande wa Jamuhuri utawasilisha mashahidi tisa na
vielelezo vya ushahidi wa ramani ya eneo la sehemu alipofia Kanumba,
ripoti ya ukaguzi wa daktari na maelezo ya onyo ya Lulu aliyopewa.
Mawakili wa utetezi ni Fuljensi Masawe, Kenedy Fungamtama na Peter Kibatala.
-Mtanzania
|
No comments:
Post a Comment