WANAOCHAFUA MAZINGIRA FELI WACHUKULIWE HATUA. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, December 27, 2012

WANAOCHAFUA MAZINGIRA FELI WACHUKULIWE HATUA.

Hivi karibuni Serikali imekua ikichukua hatua kwa wachafuzi wa mazingira hasa kwenye fukwe za bahari ya Hindi lakini bado haijamulika uchafuzi huu unaofanyika hadharani kwenye eneo la Soko kuu la Kimataifa la Samaki la Feli, Pamoja na kuwepo vyoo vizuri kwenye soko hilo lakini bado wavuvi, wachuuzi pamoja na watu wengine hawavitumii vyoo hivyo nakwenda kujisaidia kwenye maji ya ufukweni. Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya watu waliozungumza na raha za pwani wanasema tatizo kubwa ni kushindwa kulipia gharama za huduma ya Choo ambayo ni shilingi miambili (Tsh 200) kila unapokwenda kujisaidia.
Biashara kama hizi nazo za madafu, na zingine mfano wa hizo hufanyika na kuziacha takataka kwenye fukwe hizo na kuharibu kabisa haiba ya fukwe hizo.
Pamoja na mwonekano mzuri wa Soko hili lakini kiukweli linafujwa sana na watumiaji wa soko na pengine hata viongozi kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi nzuri wa usafi wa mazingira. Harufu kali za uvundo kama sio mizoga zinatawala huku majitaka yakitiririka hovyo kuelekea kwenye fukwe hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here