NILIWAHI kusikia kwa kiongozi mmoja wa dini alisema hivi “Mnaweza mkalipenda jambo na mkaling’ang’ania hali
yakua jambo hilo linamadhara kwenu lakini hamjui na mnaweza mkalichukia jambo
kwa nguvu kubwa kumbe ndio lenye faida kwenu” mwisho wa kunukuu.
Hakuna mtu anaependa kuona vurugu zikitokea
mahala popote kwani mali na maisha ya watu hupotea kama sio kupoteza viungo vya
mwili na kupata ulemavu wa kudumu. Lakini kwa mgogoro huu tumshukuru sana
mwenyezmungu kwa kutokea wakati huu kuliko ungetokea wakati miundombinu ya
mradi wa gesi ikiwa imekwisha jengwa (Laana ya gesi imetuwahi mapema kabla).
Pamoja nakwamba wataalamu wanaeleza kua
gesi asilia haina athari sana ya milipuko ikilinganishwa na aina nyingine za
gesi lakini siku kama yaleo tungekuwa tunazungumza janga la Afrika ama la
Kidunia maana na hakika kwa hasira walizokuwanazo vijana wa Mtwara
wasingeshindwa kwenda kulipua moto bomba la gesi.
Kama hilo lingefanyika bilashaka
tungelishuhudia moto ukitoka Mtwara kuelekea jijini Dar es Salaam kuliangamiza
jiji lenye wakazi zaidi ya 5Millioni. Hapa watanzania tumepata funzo kwenye
tukio hili na tujifunze kutokana na makosa.
KWANINI
MATUKIO YA FUJO YAMETOKEA SASA MTWARA? Majibu ya
swali hili niwazi sababu kubwa ya matukio hayo ya vurugu ni serikali yenyewe
kwakushindwa kushughulikia tatizo la msingi badalayake iliendelea na tabia ya
kuwa na majibu rahisi kwenye maswali magumu yanayoaambatana na kejeli.
Majibu ya kejeli ya serikali kupitia
mawaziri wake na hata viongozii wa chama tawala wa mkoa huo wamechangia
kupandisha hasira kubwa zilizokosa mtu wakuzishusha kwakutoa majibu ya kuleta
matumaini kwao kabla ya kuanza kutoa elimu kwa wananchi hao. Kwakua hakuna
aliyekwenda kuwapa elimu yoyote kuhusu yale madaiyao ilitosha ujumbe wa upande
mmoja wanaoupata kujaza ‘vakyum’ na kusubiri ipasuke tu.
Pamoja na hasira za wananchi hao kuwa
nyingi na kuonekana waziwazi kwamba wanatafutia sababu tu ili waonyeshe hasira
zao bado serikali ilikua kwenye usingizi mzito nakujisahau kabisaaa, hata pale
wanasiasa walipokwenda kunyunyizia petrol mgogoro huo hakuna aliyejali kwenda
kuondoa tatizo.
Alianza Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James
Mbatia akaonja vurugu walipomkatalia hojazake akajinasibu kisiasa kuwa ni kikundi cha watu wachache tu ndio
wanaleta fujo lakini wengiwao wamemuelewa.
Wakaja watu watanesco walipozima umeme
wakati mkutano wa wanasiasa wa upinzani ukiendelea, na mabomu yakapigwa bado
serikali ikapuuzia tu.
Akachomewa moto gari Afisa wa usalama wa
Taifa, bado tukaona kimya.
Akavamiwa diwani kwa madai ya ushirikina na
tukio la mwisho lililosababisha vifo vingi vya watu sita jana Chanzo ni Polisi
kumshikilia mwendesha bodaboda. Utaona ni wazi hawa wananchi walikua na presha
ambayo ikitafuta sehemu ya kutokea tu na hili lilishabainika na wachambuzi wa
mambo ya kijamii. Nathubutu kusema laana ya gesi imewahi kabla ya muda ili
tujifunze kwanza na namna ya kukabili matatizo yatakayokuja kujitokeza baadaye
maana ni lazima yatokee kwasababu waswahili walishasema kwenye riziki hapakosi
fitina. UCHAMBUZI WA MHARIRI RAHA ZA PWANI.
|
No comments:
Post a Comment