| Francis Cheka (kushoto) akiwa na Adam Tanaka (katikatia) na Thomas Mashali (kulia) SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa Afrika
(IBF/Africa) limetoa kibali kwa bondia Francis Cheka ambaye ni bingwa wa Africa
katika uzito wa Super Middle kutetea ubingwa wake dhidi ya bondia Thomas
Mashali wa Tanzania. Mabondia hao wawili leo tarehe 13 February walikutana
katika hoteli ya Ndekha, iliyoko Magomeni Kondoa na kutia saini mkataba wa
kupigana pambano hilo ambalo limepangwa kufanyika siku ya Mei Day katika ukumbi
wa PTA jijini dar-Es-Salaam. Thomas Mashali ambaye ndiye bingwa wa Afrika ya
Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle anakiwango kizuri cha
kushindana na Francis Cheka katika pambalo hilo. Hii itakuwa mara ya pili kwa
bondia Francis Cheka kutetea mkanda alioushinda tarehe 29 April 2012 dhidi ya
bondia machachari Mada Maugo wa Tanzania. Cheka aliutetea vyema mkanda wa
ubingwa wa IBF/Africa dhidi ya bondia Chiotcha Chimwemwe ambaye ni Afisa katika
jeshi la Malawi siku ya Boxing Day (26 Decewmber 2012) katika jiji la Arusha.
Kama Francis Cheka atashinda tena pambano hili, atapewa nafasi ya kupigana
kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C).Pambano hili linaandaliwa na kampuni
ya Mumask Investment and Gebby Pressure ya jijini Dar-Es-Salaam chini ya
uratibu wa Adam Tanaka!Imetumwa na: UONGOZI, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa
Africa (IBF/Africa), Dar-Es-Salaam, Tanzania |
No comments:
Post a Comment