POLISI mkoani Mwanza wanamshikilia Imamu wa Msikiti wa Ijumaa Imaam Hamza,
huku likitangaza kuwasaka masheikh wawili wengine pamoja na Askofu
(majina yote yanahifadhiwa) kwa kuhusika na uchochezi wa kidini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu
alisema Imamu huyo wa msikiti alitiwa mbaroni kwa madai ya kubainika
kwamba wanahusika na usambazaji wa CD za uchochezi ambazo zimekuwa
zikihamasisha vurugu pamoja na mauaji ya kidini ikiwa ni pamoja na suala
la kuchinja.
Kwa upande wake Askofu Mpemba wa Kanisa la
Tanzania Field Evangelist yeye anasakwa kutokana na kutoa mkanda wa
video (DVD) yenye jina la ‘Inuka Chinja Ule’ wakati mashehe wawili
wanasakwa kwa kuhusika na uandaaji wa mikanda ya video mitatu (DVD)
zenye majina ya ‘Unafiki katika Sensa, Kadhia ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar pamoja na Uadui wa Makafiri’.
Wakati huohuo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(Bakwata) Mkoa wa Morogoro, limesema huenda likajitenga na Bakwata Taifa
kufuatia hatua ya Sheikh Mkuu, Mufti Issa Shaaban bin Simba kumvua
madaraka Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, Yahya Semwali bila kufuata
utaratibu.

No comments:
Post a Comment