Polisi walivyo
imarisha ulinzi nje ya jengo
la Sukari lililopo mkabala na Makutano ya Barabara za Ohio na Sokoine
Driver Posta jijini Dar es salaam jengo hilo ndmo zilimo ofisi za
mwendesha mashtaka wa Serikal Dk.Eliezer Feleshi, Ulinzi huo
umeimarishwa kutokana na tishio la wafuasi wa Shekh Ponda kutishia
kuandamana kwenda kwa Mwendesha Mashtaka huyokushinikiza Shekh Ponda
aachiwe huru.
Baadhi ya
wafuasi hao wa Shekh Ponda wamekamatwa katika maeneo mbalimbali wakati
wakijaribu kuingia katika eneo la Posta ambapo ulinzi mkali uliimarishwa
huku polisi wakitumia Magari, Pikipiki, Mbwahuku makachero wakizunguka
kila mahali.
Baadhi ya
Barabara zilifungwa ili kuweka eneo hilo katika hali ya usalama zaidi na
kuhakikisha linzdhibitiwa na kulidwa kirahisi.
|
No comments:
Post a Comment