For Immediate
Release Media
Contact: Onesmo
Ngowi
Kuna hekaheka nyingi
kwenye jiji la Accra, nchini Ghana wakati wa
pambano la kugombea ubingwa wa dunia kati ya bondia marufu Joseph Agbeko
kutoka
Ghana na Luis Mendenez bondia anayetoka katika nchi ya Amerika ya Kusini
ya
Columbia watakapokutana siku ya jumamosi tarehe 8 Machi.
Kati ya mapambano ya
utangulizi bondia anayeinukia kwa kasi Richard
Commey atakutana na bondia mwenzake wa Ghana Bilal Mohammed kugombea
mkanda wa
IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika
uzito
mwepesi (Lightweight).
Wawili hao wanatoka
katika kambi mbili zinazohasimiana kwa siku nyingi
na mpambano wao unategemea kuwa wa kasi, ufundi na wenye kusisimua
katika raundi
zote 12.
Mpambano wa Richard
Commey (khttp://www.youtube.com/watch?v=IBG5a9LtIhU)
na Bilal Muhammed umekuwa gumzo kubwa katika
jiji la Accra pamoja na majiji mengine katika Afrika ya Magharibi. Hii
inatokana
na umaarufu wa promota na meneja wa Ruchard Commey Mghana Michael Amoo
Bediako
anayeishi barani Ulaya akiwa na makazi yake nchini Uingereza kuwa mtu
aneyeshughulika na mabondia wenye vipaji vya hali ya juu.
Richard Commey
atapenda kuwadhihirishia wapenzi wake kuwa yeye ndiye
Mfalme wa Afrika katika uzito wa mwepesi (Lightweight) na hakuka
atakayeweza
kumzuia katika mipango yake ya kupanda ngazi. Naye Bilal Muhammad
atapenda
kuudhihirisia ulimwengu kuwa sio bondia anayeweza kusukumwa sukumwa na
kwamba
ubingwa wa IBF AMEPG katika uzito wa Lightweight na wake.
Imetolewa na:
ISSUED BY:
INTERNATIONAL
BOXING FEDERATION AFRICA
(IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM,
TANZANIA

No comments:
Post a Comment