SIKU nne baada ya kupiga kura wakenya wangali kujua
mshindi, wa urais, baadhi ya yaliyojitokeza hadi sasa ni pamoja na
malalamishi ya muungano wa CORD wake Raila Odinga kutaka tume ya
uchaguzi kusitisha shughuli ya kuhesabu kura wakidai kufanyika
udanganyifu.Nayo tume ya uchaguzi yasema idadi kubwa ya kura zilizoharibika ilitokana na hitilafu katika mtambo wake ambao ulikuwa unaongeza idadi ya kura hizo mara nane
Matokeo hadi kufikia sasa Raila Odinga ana kura 4,516,660 wakati Uhuru Kenyatta ana kura 5,159,344
Wakenya wakiwa katika kipindi kigumu na cha wasiwasi kwani imechukua Tume ya Uchaguzi muda wa siku nne tangu kuanza shughuli ya kuhesabu kura na bado mshindi hajajulikana.
Kumekuwa na kila aina ya matukio katika muda huo wote. Tayari mashirika ya kijamii yameitaka mahakama kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura inayofanywa na tume ya uchaguzi.Muungano wa CORD unaoongozwa na tume ya uchaguzi, umelalamika ukisema shughuli hiyo ina mizengwe na wanataka ianzishwe upyaa. Mahakama kuu nchini Kenya imetupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa na mashirika ya kijamii dhidi ya tume ya uchaguzi wakiitaka isitishe shughuli ya kuhesabu kura za urais. Walidai kuwa tume hiyo inahujumu matokeo hayo.Mahakama imeyataka mashirika hayo kuiwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya juu zaidi

No comments:
Post a Comment