Waumini wa dini ya Kiisilamu wakiwa kwenye Kongamano lililofanyika leo jijini Dar es Saalaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na masheikh. Msimamo wa waisilamu juu ya Maendeleo ya mchakato wa katiba mpya, Dhulma na uonevu dhidi ya waisilamu pamoja na hatua za kuchukuwa kama madai yao yatapuuzwa.
Na Mwandishi Maalum.
WAISILAM leo wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali
yanayoendelea nchini wakati wa kongamano lililoandaliwa na jumuiya na Taasisi
za Kiisilamu Tanzania jijini Dar es Salaam.
Kwenye kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo
Sheikh Ponda Issa Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo
waliwasilisha mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo.
Moja ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha
kwenye Tume ya katiba mpya ambapo walisema iwapo mapendekezo waliyowasilishwa
hayakuzingatiwa na kutupwa yote basi waisilamu watatangaza kusimamisha mchakato
huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana.
Hoja hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa
nchi Sera na Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge
Asumta Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya
kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya wakristo
haioni inawadhulumu hakiyao yakufanya ibada?, Lukuvi kwenye jibu lake alisema
suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu lakini serikali kwenye hilo
haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga kura ila kwakuwa kuna mchakato wa
katiba mpya hilo litazingatiwa.
“Hii ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba waziri
huyu anataka tuamini kwamba anayafahamu
yatakayokuwemo kwenye katiba mpya kabra hata wananchi hawajapelekewa na hata
haijaandikwa? Hivyo iweje waisilamu wanaodai siku ya ijumaa iwe ya mapimziko
kwa miaka nenda rudi hawapewi wakristo wanakosa sikumoja tu ndani ya miaka
mitano majibu yanapatikana kirahisi?” Alihoji sheikh Ponda.
“W aisilamu wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya
ijumaa kwenda kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo lakini
hakuna vurugu yeyote waliofanya na wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii lakini
hawapewi lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.” Alifafanua.
Aidha heikh Ponda alifafanua kuwa waisilamu wavumilie
wasubiri rasimu itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali kama mapendekezo
waliyowasilishwa yatapuuzwa basi hakuna katiba mpya maandamano usiku na mchana
mpaka kieleweke nchi nzima.
Sheikh Ally Basaleh alisihi Serikali kuwasikiliza waisilamu
hoja zao wasiwapuuze.
|
No comments:
Post a Comment