JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA
MADINI
TANGAZO
KONGAMANO LA
WAZI NA UZINDUZI WA MPANGO WA KULETA MATOKEO MAKUBWA SASA KWA WIZARA YA NISHATI
NA MADINI
Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mbunge), anawaalika wadau
wote wa Sekta ya Nishati na Madini kote nchini kwenye kongamano
la wazi litakalofanyika siku ya Jumatano Julai 3, 2013 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Mwenge Jijini Dar es
Salaam, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.
Mada
kuu ni kujadili, kushauri na kutoa maoni juu ya
miradi mikubwa ya kitaifa ya sekta ya nishati itakayotekelezwa na Wizara ya
Nishati na Madini kwa kipindi cha miaka mitatu, Julai 2013 – Disemba 2015 ili
kuliwezesha Taifa kufikia Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).
Wadau wanaoalikwa ni pamoja na:
Mabenki washirika, Wakandarasi kwenye sekta ya Umeme, Wahandisi
kutoka Taasisi na Vyuo Vikuu nchini, Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya
kiserikali, Wawakilishi kutoka Makampuni mbalimbali, Migodi, Viwanda vikubwa na
vidogo na wananchi wote kwa ujumla.
Hakuna kiingilio kwenye uzinduzi huo.
“Matokeo Makubwa sasa kwa maendeleo ya Mtanzania”
Imetolewa na:
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini
No comments:
Post a Comment