Wafuasi na wapinzani wa rais wa
Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi Wanafanya maandamano makubwa
mjini Cairo mchana huu, huku waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimisha Ijumaa ya kwanza ya
mwezi mtukufu wa Ramadan.
Wafuasi wa Bwana Morsi wanatarajia
kuwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo, wataendelea kuunga mkono wito wao wa
kutaka Bwana Morsi kurejeshwa madarakani.
Wapinzani wa rais huyo wa zamani
ambao waliandamana hadi rais huyo akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika
katika medani ya Tahrir.
Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia
zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo, Jim
Muir anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood huenda liliwatenga raia wengi
wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi wa nchi hiyo hawataki jeshi
kuingilia masuala ya siasa.
Marekani
kutuma ndege za kivita Misri
Siku ya Alhamisi serikali ya
Marekani, ilitoa wito kwa utawala mpya wa Misri, kusitisha harakati zake za
kuwakamata wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood na kuonya dhidi ya
kulenga kundi lolote.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki Moon vile vile ameonya utawala huo wa Misri kutotenga chama chochote cha
kisiasa katika harakati za kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa hilo.
Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya White
House, Jay Carney amesema, utawala wa Washington hauamini kuwa ni lazima
isitishe misaada yake ya Misri.
Marekani inatarajiwa kupeleka ndege
nne za kivita aina ya F-16 nchini Misri, lakini haijathibitisha kuwa msaada huo
utatolewa lini.
Serikali ya Marekani imesema,
inachunguza ikiwa aumuzi huo wa jeshi la Misri kumuondoa madarakani rais Morsi
ni mapinduzi ya Kijeshi kwa kuwa sheria za Marekani inazuia serikali kutoa
misaada kwa nchi yoyote ambayo kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia
ataondolewa kupitia mapinduzi.
Wafuasi wa rais Morsi wamekuwa
wakiandamana wiki nzima karibu na kambi ya kijeshi iliyoko Mashariki mwa mji
mkuu wa Cairo, ambako wanaamini kuwa kiongozi wao anazuiliwa na maafisa wa
kijeshi tangu alipoondolewa madarakani.
|
No comments:
Post a Comment