Muhammad
bin Siriyn amesema, "Abu Huraryah amesimulia Hadiyth hii na akasema:
"Huyu ni mama yenu enyi wana wa maji ya mbinguni" (yaani Waarabu kizazi
cha Ismaa'iyl عليه السلام, mwana wa Haajar ambaye ndiye aliyesababisha
maji ya Zamzam). [Fat-h Al-Baariy 6:447, Muslim 4:1840] Mke wa Ibraahiym عليه السلام Sarah, alikuwa tasa. Na Ibraahiym عليه السلام alikuwa anazeeka na nywele zake zikatawaliwa na
mvi baada ya kuita watu miaka mingi katika dini ya Allaah. Sarah
akafikiria kwamba yeye na Ibraahiym عليه السلام wako katika upweke kwa
vile hawakupata mtoto. Kwa hiyo akampa mumewe mtumwa wake Haajar amuoe.
Haajar akamzaa Ismaa'iyl عليه السلام ambaye ndiye mtoto wa mwanzo wa
Ibraahiym عليه السلام. Siku zikapita na Ibraahiym عليه السلام
akawa na furaha ya kupata mtoto, lakini Sarah akawa na wivu sasa na
Haajar, ingawa yeye mwenyewe ndiye aliyempa Ibraahiym عليه السلام Haajar
amuoe. Wivu huo ukamfanya Haajar awe anajificha ili Sarah asimuone
anapokwenda kwa mumewe. Akawa ni mwanamke wa kwanza kufunga mkanda
kuficha alama zake kama ilivyotajwa katika Hadiyth ndefu kutoka kwa
Al-Bukhaariy iliyopokelewa na Ibn 'Abbaas kwamba "Haajar ni mwanamke wa
mwanzo kutumia mkanda". Makusudio hapo ni mkanda kiunoni kuzuia
nguo yake ndefu inayoburuza ardhini isiache alama apitapo (ikaja
ikajulikana na Sarah kuwa kapita). Inasemekana kuwa wakati huo wanawake
walikuwa wakivaa nguo ndefu zinazoburuza. Na hii inaonyesha jinsi stara
ilivyokuwa kwa wanawake tangu wakati huo. Pia katika masimulizi
kwenye Sahiyh Al Bukhaariy anasema, ''Wakati Nabii Ibraahiym عليه
السلام alipomuoa Haajar na akamzalia Ismaa'iyl عليه السلام, mkewe wa
mwanzo, Sarah, akapata wivu na akaapa kuwa atamkata mwili wake vipande
vitatu, hivyo Haajar akajifunga mkanda kiunoni mwake na kukimbia huku
akiburuza vazi lake nyuma yake ili kufuta alama za nyayo zake ili Sarah
asiweze kujua alipoelekea. (Al Bukhaariy - Kitabu cha Visa Vya Mitume,
hadiyth namba 3364) Na Allaah Anajua zaidi.
|
No comments:
Post a Comment