Umoja wa Ulaya
umemtunuku Mama, Helen Kijo- Bisimba (pichani), kutokana na mchango wake
kwa ajili ya kutetea na kulinda haki za binadamu nchiini.
Tuzo
hiyo, ilitolewa juzi na EU siku ya Jumanne wiki hii jijini Dar es
Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Maendeleo Ulaya 2015.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya bwana, Filberto Sebregondi, alitoa tuzo hizo na kusema
kuwa lengo lake ni kusimamia haki kwenye masuala ya kiulimwengu ikiwemo
kupambana na umasikini na kuhamasisha raia kujihusisha na maendeleo.
Wengine waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo pamoja na Mama Bisimba ni wanamziki
Keisha Shaban, Fareed Kubanda (FID Q), na Balozi Ami Mpungwe, pamoja na Paul Ndunguru ambae ni msanii na mchoraji.
EU
imekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki za
binadamu hususani ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ikiwemo vitendo
vya ukeketaji, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe.
Vilevile, EU imekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kupinga adhabu ya kifo. |
No comments:
Post a Comment