|
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipitia kijarida cha
maelezo kazi zinazofanywa na taasisi inayoshughulikia na utetezi wa
watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati
2014/15. Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Doris Mollel wakati wa
hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki
kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar. |
Na Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kubadili utamaduni na kumshikirisha mwanamme wakati mke wake akienda kujifungua ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na mama.
Alisema wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.
Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa wiki.
Alisema yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume kukalishwa chini kuelekezwa.
|
Muuguzi wa
wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda
akitoa somo na elimu ya makuzi kwa watoto njiti wanaozaliwa nchini
kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
Aidha
ushiriki wa wanaume katika ujauzito umeelezwa kusaidia kuondoa
mashinikizo na ukosefu wa lishe bora kwa wawanake wajawazito kutokana na
vitu hivyo kuwa sehemu ya uzazi wa watoto njiti.
Alisema
pamoja na kutoa elimu kwa wanaume na wanawake hasa wauguzi juu ya haja
ya wanaume kuona mahangaiko ya wanawake zao, ameitaka jamii kutambua
kwamba uzazi katika umri mdogo ni tatizo jingine linalopsababisha uzazi
wa watoto njiti.
Alisema
kuhusu mabadiliko katika hospitali na zahanati zetu ili kuwa bora kwa
uzazi salama Naibu waziri huyo alitaka taasisi mbalimbali kushirikiana
na serikali kuhakikisha kwamba si watoto njiti tu wanakuwa salama bali
hospitali na zahanati hizo zinakuwa salama kwa uzazi wa aina zote.
Awali
wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua taasisi hiyo, Balozi
Mwanaidi Sinare, alisema kwamba ipo haja ya zahanati na hospitali za
Tanzania zikawa katika hali ya kupokea uzazi wa aina zote ili watoto
njiti waweze kuendelea kuishi. |
|
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahmoud
Thabit Kombo, akizungumza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel
uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Wakati
huo huo mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wake, Doris
Mollel ambaye ni Mrembo wa Singida 2014/15, ambaye alisema yeye
alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2. Molel alisema zaidi ya watoto
200,000 huzaliwa njiti kila mwaka huku elfu 9 wakifariki.
Alisema
wengi wa watoto hao hufariki kwa kukosa huduma muhimu hasa mashine za
kuwawezesha kunyonya, kupata joto kuendelea kuishi kabla ya kutoka
hospitalini.
Alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia watoto njiti ili kupunguza vifo na kuviondoa.
Watoto njiti milioni 15 huzaliwa duniani na kati yao milioni 1 hufa wengi wao kutoka nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na
utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda
ya Kati 2014/15, Doris Mollel akielezea makuzi yake baada ya kuzaliwa
njiti wa uzito wa kilio 1.2 na kuona kuna umuhimu wa kusaidia watoto
njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao
waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa
na wakiwa njiti. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na
utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda
ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimpongeza Balozi Mwanaidi Sinare kwa
risala nzuri aliyoitoa wakati wa sherehe za uzinduzi wa taasisi hiyo
uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency mwishoni mwa wiki jijini Dar.
Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
|
|
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo
akizungumza na kumpongeza Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi
wa taasisi hiyo. |
|
Meza kuu wakijianda kuelekea sehemu maalum ya kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na
utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda
ya Kati 2014/15, Doris Mollel na mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena
Mujtaba kwa pamoja wakikata utepe kuzindua taasisi yao huku Naibu Waziri
wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo
(kushoto) na Balozi Mwanaidi Sinare wakishuhudia tukio hilo. |
|
Sasa imezinduliwa rasmi. |
|
Balozi
Mwanaidi Sinare (kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa taasisi
inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia
ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel kwenye uzinduzi huo.
|
|
Sehemu ya ndugu, jamaa na marafiki
waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni
mwa wiki kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo. |
|
Meza kuu kwa pamoja wakikata cake maalum wakati wa uzinduzi huo. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na
utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda
ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake mgeni rasmi Naibu Waziri
wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo
wakati wa uzinduzi. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na
utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda
ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Balozi Mwanaidi Sinare. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa
watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati
2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Muuguzi wa wodi ya watoto
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda (kushoto). |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na
utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida
Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mshirika
mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na
utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda
ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mama yake
mzazi Celina Mollel. |
|
Rachel Temu, William Malecela pamoja na mdau wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. |
|
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo
(kulia) Mdau wa Doris Mollel Foundation, Suleiman Saleh pamoja mgeni
mwalikwa. |
|
Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania,
Hoyce Temu (kushoto) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa taasisi ya
Doris Mollel. Kulia ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi (kulia). |
Mtangazaji wa kituo cha Channel Ten na Magic FM, Salma Msangi na rafiki yake wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts ambao ni Wachapishaji wa Magazeti ya Jambo Leo, Juma Pinto (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, Benny Kisaka (wa pili kulia) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo.
Mama mzazi wa Doris Mollel , Bi. Celina Mollel (kushoto) katika picha ya pamoja na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Ramesh Patel.
|
Mjasiriamali Maznat Yusuph Sinare
(aliyesimama katikati) akiteta jambo na Balozi Mwanaidi Sinare (kulia)
kwenye sherehe fupi za uzinduzi wa Doris Mollel Foundation. |
|
Balozi Mwanaidi Sinare akisalimiana na Mh.
Iddi Simba (aliyeipa mgongo kamera yetu) Kulia ni mgeni rasmi Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo. |
|
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti
ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris
Mollel akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya
Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kushoto) Balozi Mwanaidi
Sinare pamoja na mshirika mwenza wa taasisi ya Doris Mollel, Heena
Mujtaba. |
|
Pichani juu na chini ni Doris Mollel na
familia yake akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria
uzinduzi wa taasisi yake. |
|
Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Rafiki wa Doris Mollel ambaye ni Mlemavu Sophia. |
|
Kutoka kushoto ni Msanii wa filamu nchini,
Sinta, Hoyce Temu pamoja na Rachel Temu wakipiga picha kumbukumbu mara
baada ya uzinduzi huo kufikia tamati. |
|
Doris Mollel na Sintah. |
|
Mdau Chiku Lweno (kulia) akipozi na Doris Mollel pamoja na baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo. |
No comments:
Post a Comment