Kampuni moja ya kutengeza madawa imelazimika kujitetea vikali baada ya kupandisha gharama ya dawa ya Ukimwi kwa asilimia 5,000.
Hii inamaanisha kuwa bei ya tembe moja ya dawa inayotumika kupunguza makali ya ukimwi itapanda kutoka dola $13.50 hadi $750.
Kampuni
hiyo inayoitwa Turing Pharmaceuticals imelaumiwa na washika dau wa
maswala ya Ukimwi kwa kuongeza bei ya dawa hiyo ya Daraprim ambayo
imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uwezo wa mwili wa mgonjwa
aliyeathirika kupigana na maambukizi mapya.
Turing Pharmaceuticals ilinunua hati miliki ya dawa hiyo ya Daraprim mwezi uliopita Agosti.
Mkurugenzi
mkuu wa kampuni hiyo Martin Shkreli amenukuliwa akisema kuwa faida
itakapatikana baada ya mauzo ya dawa hiyo itasaidia kugharamia utafiti
wa dawa mpya na zenye ubora zaidi.
Tembe moja ya dawa hiyo ya Daraprim inagharimu dola moja pekee kutengeneza.
Hata hivyo bwana Martin Shkreli anasema kuwa bei hiyo haijumuishi
gharama ya kunadi dawa hiyo wala usambazaji wake ilihali gharama
imeimarika maradufu katika miaka ya hivi punde.
''Katika siku za
hivi punde dawa za kupunguza makali ya saratani zinagharimu dola laki
moja (100,000) ilhali gharama yake asili inaweza kugharimu dola nusu
milioni.
Daraprim inauzwa kwa bei nafuu zaidi ikilinganishwa na dawa zinazotibu magonjwa sawa.
Shkreli aliiambia runinga ya Bloomberg katika mahojiano ya kibinafsi.
Shkreli
alimsuta mwandishi mmoja wa habari kupitia mtandao wa Kijamii akimuita
kuwa ''mjinga'' kwa kutaka kujua kwanini kampuni yake ilikuwa inaongeza
maradufu bei ya dawa hiyo muhimu katika vita dhidi ya Ukimwi haswa
katika mataifa maskini duniani.
Daktari Wendy Armstrong kutoka muungano wa wauguzi nchini Marekani
HIV Medicine Association amekashifu sababu zilizotolewa kwaajili ya
nyongeza hiyo kubwa ya bei ya dawa hiyo.
Muaniaji tikiti cha urais
wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameonya kuwa serikali yake
itachukua hatua kali dhidi ya makampuni yanayofaidi kutokana na msiba wa
watu kwa kupandisha bei ya madawa maalum.
No comments:
Post a Comment