Hayo yameelezwa na wakazi wa Kisarawe mkoani
Pwani jana wakati wa mdahalo wa amani uliondeshwa na kusimamiwa na Chama Cha
Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).
Katika mdahalo huo ambao mada kuu ilikuwa ni
umuhimu wa amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
Mada nyingine zilizojadiliwa ni Haki ya mwanamke
kushiriki kupiga kura kwnye uchaguzi mkuu, pamoja na elimu ya mpiga kura na
Haki za Binadamu.
Akichangi mada wakati wa mdahalo huo ambao
ulishirikisha wenyeviti, watendaji wa Serikali za mitaa, Jeshi la Polisi na
Watumishi wa halmashauri hiyo, Mwashamba Mrisho,alisema kutokuwepo kwa haki
wakati na baada ya uchaguzi ni moja ya vyanzo vya kuvuruga amani.
"Kama haki haitendeki basi ni vigumu sana
amani kupatikana, kwa mfano kama watendaji au wasimamizi wa uchaguzi watafanya
upendeleo wa kufanya mikutano kwa baadhi ya vyama na kuvinyima haki hiyo kwa
baadhi ya vyama kunaweza kubomoa amani iliyopo," alifafanua Mwashamba.
Aidha wananchi hao walibainisha kuwa vyanzo
vingine vya vurugu kuwa ni matumizi ya lugha ya matusi pamoja na kutangaza
mgombea ambaye hakushinda na kumwacha mgombea aliyeshinda.
Awali akifungua mdahalo huo mwakilishi wa Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Mtendaji wa Tarafa ya Chole, Asha Risasi,
alisema kuna umuhimu watendaji wa serikali za mitaa na wananchi kujua majukumu
ya Mkuu wa Wilaya kwani wao wako karibu zaidi na wananchi hivyo itasaidia
kufanya kazi kwa ushirikiano.
"Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama
kwenye Halmashauri ni Mkuu wa Wilaya na yeye ndio mwenye vyombo vya kulinda
amani kama Jeshi la Polisi, Takukuru na Magereza, hivyo kuna umuhimu wa
wananchi pamoja na watendaji kuelewa hilo ili kurahisisha utendaji wao,"
alieleza Risasi.
Akitoa nasaha zake kwa washiriki wa mdahalo huo
Afisa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo, Constantine Mnemere, alisema kuwa uchaguzi
sio vita ni mchakato halali wa kisheria unaolenga kupata viongozi watakao
simamia maslahi ya wengi na hakuna sababu ya wananchi kufarakana nakuvuruga
amani iliyopo.
Akieleza kwanini wameamua kufanya mdahalo huo kwa
watendaji wa serikali za mitaa, watumishi wa Halmashauri na wananchi, Ofisa
Habari wa Tawla, Goodness Mrema, alisema kuna kila sababu ya kufanya hivyo
katika jamii kwani wananchi wanaingia kwenye uchaguzi wanapaswa kukumbushwa
umuhimu wa amani na umuhimu wa kushiriki kupiga kura.
"Tuko atika juhudi za kuimarisha Utawala
Bora katika jamii na hii ndio itakuwa chachu ya kuimarisha amani itakayowezesha
wananchi kushiriki katika uchaguzi kwa amani na hatimaye kupata viongozi
bora," alisema
Aidha Mrema alisema wanafanya midahalo hiyo kwa
ngazi ya chini ya uongozi kwakuwa wanaamini kuwa wako karibu zaidi na wananchi
na kwakufanya hivyo itasaidia kurahisha kufikisha ujumbe wao.
No comments:
Post a Comment