Mahakama kuu nchini Mexico imetoa amri ya kuliruhusu kundi la wanaharakati kupanda na kusambaza bangi kwa matumizi yao wenyewe.
Hata hivyo kauli hiyo itafanya kazi wa wanne hao waliokwenda mahakamani pekee yao.
Wataalamu wanasema kuwa amri hiyo huenda ikafungua milango itakayoruhusu na kuhalalishwa matumizi ya bangi siku zinazokuja.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kuwa amri hiyo inazua mjadala kuhusu njia za kudhibiti matumizi ma usambazaji wa madawa ya kulevya.
Wanaharakati wanasema kuwa kushindwa kwa Mexico kuhalalisha matumizi ya bangi ndiko kulikowawezesha walanguzi wa mihadarati kukolea katika biashara hiyo na kujivunia mabilioni ya fedha katika faida.
No comments:
Post a Comment