Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza na Wananchi walio fika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata vipimo na kupatiwa ushauri na Madaktari kutoka Hospitali Mbalimbali Jijini Dar es Salaam
Wananchi wakiwa na watoto wao katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Wananchi wakiwa katika mistari ambao hawajapata namba
Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma Mfinanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Zoezi la kupima vipimo kwa wananchi bure lililo ratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Hospitali mbalimbali za Dar es Salaam ikiwemo, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aga Khan Hospital, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ikiongonzwa na Rais wa Chama cha Madaktari Figo Tanzania na pia ni Daktari Bingwa wa Figo Dk. Onesmo Kisanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grece (kushoto) Magembe akiwaonyesha jambo wananchi walio jitokeza kupata huduma ya vipimo kutoka kwa Madaktari wa Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili mkoa wa Dar es Salaam ilioratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini humo na kutokana na mwitikio wa wananchi huwenda ziku zitaongezwa baada ya Mkuu huyo kujadiliana na madaktari hao ambapo Septemba 25 hapo awali ilikuwa ndio siku ya kuhitimisha zoezi hilo
Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja
Zuhura Shaba (54) akiwa amebebwa na baadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Afya baada ya kujikuta amepoteza fahamu mara baada ya kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam , baada ya muda na mpiga picha hizi alibahatika kuongea nae na kuanza kusema kwa utaratibu kinacho msumbua na kueleza mengi baada ya kumdadisi alisema, yeye ni Mtoto wa 7 na baba yake ezi za uhai wake miaka ya nyuma aliwahi shika nyadhifa mbalimbali Serikalini kama, Waziri wa Afya, Meneja Mkonge Tanga, aliwahi kuwa Mbunge, hivyo anamshukuru Mkuu wa Mkoa na Mungu amuongoze kwa kila anachokifanya kwa Jamii ya Kitanzania na kumshukuru Rais wa Tanzania kwa kumpa maona ya kumchagua kijana huyu, Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa na kuishukuru timu nzima ya Madaktari kwa moyo wao kuona jamii ya kitanzani bado inahali duni na kushirikiana na Mkuu wa Mkoa kutuletea zoezi hili, nashukuru baada ya kujikuta napoteza fahamu nimejikuta nipo katika chumba huduma ya haraka na kupata huduma na sasa najiona ninanafuu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi Sophia Mjema (kushoto) akishiriki zoezi la kugawa namba kwa wananchi walioitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamenyoosha mikono wakitarajia kupata namba kwa ajili ya kupatiwa huduma ya vipimo
Askari Polisi akizungumza na baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Joice Mgeta akipatiwa vipimo na Dk. Danieli Chacha (kushoto) mara baada kujikuta anaishiwa nguvu ghafla akiwa katika foleni ya kusubiri kupata namba , kulia ni Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma Mfinanga
PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA
No comments:
Post a Comment