Katibu wa Chama cha Riadhaa mkoani Tanga(RT) Hassan Mwago mba akizungumza na waandishi wa habari leo
kuishukuru kampuni ya Mkwambi Group of Campainers kufadhili mashindano
ya Riadhaa Mkoani Tanga ya Tanga City Marathon yatakayo fanyika April
15 mwaka huu katikati ni Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho kulia
ni Meneja Mkuu wa Mkwabi Group Of Campainers,Kawkab Hussein
Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho akisistiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkoanoi Tanga leo |
Sehemu ya Waandishi wa
Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua
matukio
Sehemu ya Waandishi wa
Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua
matukio
Sehemu ya Waandishi wa Habari
Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua
matukio
KAMPUNI ya Mkwabi Super Market
imejitosa kudhamini Mashindano ya Tanga City Marathon kwa kuwekeza kiasi
cha sh.milioni 16 ikiwa ni mkakati wa kurudisha hamasa na kuinua mchezo
huo mkoani Tanga
Hatua ya Kampuni hiyo ambaye
imekuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi mbalimbali za michezo mkoani
Tanga imelenga kurudisha hamasa na ushindani kwa washiriki.
Akizungumza na wandishi wa habari leo Mratibu wa Mashi ndano hayo Juma Mwajasho alisema mbio hizo zitaanza kutimua vumbi Aprili 15 mwaka huu katika Jiji la Tanga.
Mwajasho alisema mashindano hayo yatasaidia kuongeza ari ya michezo na kuamsha hamasa za wapenda riadha katika mkoa wa Tanga na lengo ni kukuza michezo huo ambao utakuwa endelevu.
Alisema washiriki wa mashindano hayo kuanzia watoto wa miaka 12 kuendelea ambao watakimbia mbio za kilometa tano,10,21, ambapo Mkwabi Super makert .
Alisema mbio za kilometa tano fomu ya usajili itakuwa shilingi
1000,mbio za kilometa 10 sh 5,000 na mbio za kilometa 20 fomu itakuwa sh 8,000 ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Tsh milion 10 na mshindi wa pili shilingi laki 700,000,mshindi wa tatu na wanne watapokea Tsh 500,000 na washindi wengine watapata kifuta jasho kila mmoja laki moja.
Katibu mkuu wa chama cha riadha mkaoa wa Tanga Hassan Mwagomba alisema mashindano hayo kwao ni faraja hivyo wameyapokea kwa moyo nakwamba wataunga mkono juhudi hizo ili kuweza kufanikiwa mbio za Tanga City marathoni mwaka huu wa 2017 .
Mwagomba alieza kuwa mashindano hayo ya mbio yataanzia katika eneo la Mkwabi Super Makert na kuzunguka kwaminchi,kisha kuishia katika uwanja wa mkwakwani.
Alisema lengo kubwa la mashindano hayo ni kufufua riadha mkoani hapa ili kuweza kuleta mafanikio na yatashirikisha wananchi wa mkoa mzima kwenye halmashauri 11 na yatakuwa endelevu.
‘’Tunatarajia kupata wataalam kutoka jijini Dar es salaam watakao wapima afya zao na usajili tayari umekwisha anza kwani zimebaki siku chache hivyo tuko kwenye hatua nzuri ya maandalizi’’alisema Mwagomba
No comments:
Post a Comment