Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI.
Na Khamisi Mussa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI Dkt, Respicious Boniface amefanya mikutano na Watumishi wa MOI Dar es Salaam jana kwa makundi kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi
Dkt, Boniface amekutana na Watumishi wa idara ya utumishi ,Uuguzi na ufundi. ambapo amewapongeza kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na alikutana na watumishi wa idara ya Tiba Kwa upande wao Watumishi wamempongeza Dkt, Boniface kwa kuaminiwa na kupewa dhamana ya kuiongoza Taasisi ya MOI
Aidha, Dkt Boniface amewaomba Watumishi wa MOI kumpa ushirikiano kwa kutimiza wajibu na kufanya kazi kwa bidii ambapo aliwaeleza kwamba changamoto zilizotolewa atazifanyia kazi na kuzishughulikia
“Nafahamu changamoto ni nyingi sana, nawaahidi kuzishughulikia kama si zote basi kwa asilimia kubwa , lengo ni kuhakikisha Taasisi yetu ya MOI inasonga mbele na inaendelea kutoa huduma bora’’
Awali Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu (MB) alimteua Dkt Lespicious L. Boniface kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) , uteuzi huo ulianza tarehe 5/04/2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili MOI, Dokt. Respicious Boniface (kushoto) akiandika jambo wakati wa Mkutano na Wafanyakazi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha, kuanzia kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Taasisi hiyo, Flora Kimaro na Meneja Uhusiano na Ustawi wa Jamii wa Taasisi hiyo, Jumaa Almasi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili MOI, Dokt. Respicious Boniface akizungumza jambo katika Mkutano na wafanyakazi wa Taasisi hiyo Dar es Salaam jana
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza kwa umakini
Mfanyakazi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI, Tula Gadi akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Mkurugenzi Mtemdaji wa Taasisi hiyo alipokuwa akizungumza nao kwa lengo la kujitambulisha kwao
Mmoja wa wafanyakazi , Fidelis Minja akizungumza jamo wakati wa Mkutano wa Mkurugenzi Mtendaji na wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI
Wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba wakiwa katika Mkutano huo
Mmoja wa wafanyakazi Bahati Mrema akizungumza katika Mkutano huo Dar es Salaam jana. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog
No comments:
Post a Comment