MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema vita ya madawaya
kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha
inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.
Akizungumza
katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya
Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Comperence
Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Alisema
vijana wengi wamekuwa wakiathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na Taifa
kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna
njia ya upitishaji.
“Kuna
wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao lakini kuna wagonjwa wengine wa
akili wa kujitakia ambao sababu zake ni matumizi ya madawa ya kulevya” alisema
Shighela na kuongeza
“Ili kuwaokoa
vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama
kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya” alisema
Kwa upande
wake Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Karstand, amewataka watumishi wa
hospitali ya Bombo kulitunza jengo hilo kama ilivyo matumizi yake.
Alisema
Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kijamii
ikiwemo Afya, elimu, Mazingira pamoja na
wagonjwa wa Afya ya Akili.
“Niuombe
uongozi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hili kwa kutumika matumizi yake
kama ilivyokusudiwa, Norway itaisaidia Tanzania kila ambapo kunahitajika
msaada” alisema
Nae Mganga
Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alisema awali wamekuwa wakikumbana na changamoto
mbalimbali ikiwemo kukosa uwezo wa kuwasafirisha wagonjwa kwenda vituo
vinavyotoa huduma za Afya ya akili.
Aliwataka
wafadhili wengine kuiga mfano wa Norway kuisadia hospitali hiyo kutokana na
changamoto ambazo imekuwa ikabiliana nazo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza kulia, Hanne-Marie Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita (kushoto) wakifungua jengo la Afya ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na kituo cha Tanga International Comperence Centre Tanga
Habari kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929
No comments:
Post a Comment