Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machema (kushoto), akishiriki zoezi la usafi pamoja na Wananzengo wengine wa Kata hiyo katika Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
Wananzengo wa Kata ya Buzuruga wakiwa pamoja na diwani wao, Richard Machema (mwenye kofia), katika zoezi la usafi kwenye Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
Zoezi la usafi la kuondoa vichaka na taka katika mazingira ya Kituo cha Afya Buzuruga limeelezwa kusaidia kuteketeza maficho ya masalia ya mbu pamoja na baadhi ya vijana wasio na maadili mema waliokuwa na desturi ya kujificha kwenye vichaka hivyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo uvutaji wa bangi.
Uteketezaji wa taka hatarishi ikiwemo chupa umelalamikiwa na wakazi wa Kata ya Buzuruga na kuomba suala hilo kufanyiwa kazi ili kuwa na uteketezaji taka usio hatarishi katika jamii
Usafi ukiendelea
Usafi ukiendelea
Mwananzengo wakiongea na Lake Fm kuhusiana na usafi huo
No comments:
Post a Comment