Na Ahmed Abdullaziz Lindi.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mama mmoja Sabina Silvestre, mkazi wa kijiji cha
Mtandi, wilaya ya Kilwa Mkoani LINDI, amemchoma moto mikono yote miwili mwanaye
wa kumzaa mwenye umri wa miaka minne kwa madai ya kuiba boga.
Mama huyo
amedai kuwa baada ya kubaini mwanaye amechukua boga bila kuomba akamchukua na
kumfunga kamba mikononi pamoja na majani makavu kisha akachukua
kibiriti na kuuwasha moto katika mikono ya mwanaye na kuuanza kumuunguza.
Mtoto huyu
mwenye umri wa miaka minne anayejulikana kwa jina la Noel John, amechomwa
moto mikono yake miwili na mama yake mazazi kwa madai ya kuiba boga, na kisha
kumficha ndani kwa siku tano bila kumpeleka hospitali ,ndipo wasamaria wema
wakatoa taarifa kwa Afisa Mtendaji Kijiji cha MTANDI Makarani Mjaka.
"Ni
kweli ndugu mheshimiwa mama huyo amemchoma moto mwanaye kwa kumfunga na majani
makavu mimi nilipata taarifa kutoka kwa raia wema nilipofika nyumbani kwake ni
kweli nikamkuta mama huyo akiwa na mwanaye, nikamuhoji akakubali kuwa amefanya
hivyo, mimi kama mtendaji nikamchukua hadi ofisini kwa mahojiano zaidi na baada
ya hapo nikampeleka katika mahakama ya hapo kijijini kwa taratibu zingine , kwa
upande wangu nilifanya hivyo kama mtendaji, pia mtoto nilimpeleka hospitalini
kwa matibabu na ameanza kupata tiba na kuandikiwa sindano tano na gharama ni
yangu mimi mtendaji wa kijiji cha Mtandi.
Mama mzazi wa mtoto huyu Sabina Silvester,alieleza kilichomsibu Alichukua
boga kwa shemeji yangu na kulileta nyumbani, akanambia mama shemeji kakupa boga
upike, mara shemeji yake akatokea na kuchukua boga, mama huyo akamuuliza
mwanaye mbona ulichukua boga bila kuomba mtoto akanyamaza kimya, mara pili tena
kamuuliza mtoto kanyamaza kimya ndipo mama huyo akamkamata mwanaye akachukua
majani makavu na kamba akamfunga mikononi kisha akachukua kibiriti akawasha na
moto ukawaka mtoto ndio hivyo akaanza kuungua.Sijampeleka hospitali nilikuwa
nampa mitishamba tu kwa sababu hela sikuwa nayo.
Bila woga
akasema Mimi naomba nawaomba akina mama wenzangu wenye roho mbaya kama mimi
wasifanye hivyo kama mimi, waache, mimi najiuliza ni kwa nini lifanya hivyo kwa
mwanangu
JOHN RAFAEL
Baba mazazi wa mtoto huyu anadai wakati tukio linatokea hakuwepo lakini
mmh Mimi nilikuwa shambani niliporudi nikamkuta mtoto yuko hivyo,
nikamuuliza mke wangu kwa nini umefanya hivyo akanijibu kwamba mtoto huyu si
wako, sasa mimi baada ya mke wangu kunijibu hivyo kikapata hasira nikaondoka
zangu, kurudi nakuta mtendaji amempeleka mtoto hospitali namshukuru sana.
Kwa upande
wao majirani wanaoishi karibu na mama huyo wamesikitishwa na kitendo hicho na
kuomba sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wanawake wanaofanya ukatili kwa
watoto
Mwajuma
Said- Mama huyu achukuliwe hatua kabisa haiwezekani mtoto kwanza alimpiga sana
kaona haitoshi kamchoma moto anatuzalilisha akina mama wenzake hapa kijijini,
hana huruma ni mkatili sana yaani alidiriki kuchukua majani makavu na kumfunga
nayo mtoto na kumuwashia kibiriti.
Rashid
Sufiani- Jamii isiwachukie watoto na kuwafanyia vibaya kama mama huyo, watoto
pia wana haki kama ilivyo kwa watu wazima wasiwapige, akina mama acheni
ukatili.
Asha
Juma- Mimi kama mtoto naomba akina mama wasituchome moto
Pia mwendesha mashitaka huyo alidai kwamba kutokana na
kitendo hicho,mshitakiwa amemsababishia mlalamikaji maumivu makali kwenye
mwili wake.
Aidha,Mwahija aliiambia mahakama hiyo kwamba kutokana
na kitendo hicho mshitakiwa amefanya kosa chini ya kifungu cha 225 kanuni ya
adhabu sura ya 16.
Mshitakiwa amekana kosa linalomkabiri na amepelekwa
rumande,baada ya upande wa mashitaka kupinga dhamana kwa mshitakiwa kutokana na
kutopata taarifa ya maendeleo ya mlalamikaji,kesi hiyo namba 49/2012,itatajwa
tena Juni 11 mwaka huu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment