![]() |
Mahali ambapo Newala inapatikana kusini mwa Tanzania picha ya Setlite. |
Watalii wakinywa Chai kwenye moja ya vijiji vya Newala. |
MFUKO wa
maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wananchi wakijiji cha Mpalu, kata ya Chitekete, wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara,wamekamilisha ujenzi wa Zahanati yao ya kijiji,na hivyo kuwapunguziakero ya kufuatilia huduma za afya mbali na maeneo yao.
Hayo yamelezwa
na Mganga mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Ndungile Yudasi, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Ofisini kwake mwishoni mwa wiki.
Dk,Yudasi
amesema kwamba kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati hiyo, kutawasaidia kuwapunguzia adha kwa wakazi wa kijiji hicho na majirani zao kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo za afya.
Mganga huyo amesema
kukamilika kwa ujenzi huo na kuanza kutoa huduma kwa zahanati hiyo, kunaifanya wilaya ya Newala sasa kuwa na jumla ya zahanati 31 zinazotoa huduma za afya kwa wakazi wilayani humo, ambapo alidai kuwa hazitoshi na kwamba juhudi zaidi za pamoja zinahitajika kuongeza nyingine.
Aidha,mganga
mkuu wa wilaya hiyo, amesema katika bajeti ya mwaka huu halmashauri ya wilaya imepanga kujenga zahanati nyingine tano na kituo kimoja cha afya cha kata ya Mkwedu ili kusogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi na kuwaondolea tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo vijiji vingine.
“Hadi sasa tuna
zahanati 31, hospitali moja na vituo vya afya vitatu
ambapo moja kati ya hivyo ni cha mtu binafsi,,,,,,,,,sasa ukilinganisha na idadi ya watu na vijiji utaona kwamba havitoshi ndio maana katika kila bajeti ya mwaka tunaongeza kujenga zahanati na vituo vya afya na kwa mwaka huu wa fedha tumepanga kujenga zahanati tano na kituo kimoja cha afya," Alisema Yudasi.
ambapo moja kati ya hivyo ni cha mtu binafsi,,,,,,,,,sasa ukilinganisha na idadi ya watu na vijiji utaona kwamba havitoshi ndio maana katika kila bajeti ya mwaka tunaongeza kujenga zahanati na vituo vya afya na kwa mwaka huu wa fedha tumepanga kujenga zahanati tano na kituo kimoja cha afya," Alisema Yudasi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment