JAMANI SENSA YA MWAKA HUU KAZI IPO UMESIKIA HILI? - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, August 24, 2012

JAMANI SENSA YA MWAKA HUU KAZI IPO UMESIKIA HILI?

Moto wa kugomea sensa unazidi kuchochewa kuni. Sheikh Ponda awatangazia utaratibu Waisilamu. Maandamano kufanyika nchi nzima wiki ijayo.
 Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiisilamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika Augost 26 mwaka huu, ambapo alisema waisilamu kamwe hawatashiriki zoezi hilo na watakaa itikafu misikitini usiku wa Augost 25 na kusoma dua mpaka asubuhi.
 Masheikh zaidi ya 40 ktoka kwenye taasisi na jumuiya na mabaraza ya kiisilamu nchini ambao pia ni maimamu wa misikiti mbalimbali jijini Dar es Salaam wakiwa wakimuunga mkono Katibu wa taasisi na Jumuiya za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakati akitangaza maelekezo kwa waisilamu juu ya namna ya kuwajibu makalani wa sensa.
 Miongoni mwa mabango ambayo yamesambazwa kwa waisilamu kotenchini kupinga kuhesabiwa kwenye zoezi la Sensa nchini.
 
Maimamu na masheikh hao wakifuatilia kwa makini tamko la sheikh Ponda mbele ya waandishi wa habari.

KATIKA kile kinachoonekana kuikomalia serikali kwenye suala la sensa taasisi na jumuiya za kiisilamu Tanzania (T) leo imetoa utaratibu wa kufuata kwa waisilamu kuanzia usiku wa kuamkia siku ya sense.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Taasisi na Jumuiya za kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda amesema wametoa maelekezo kwa waisilamu wote nchi nzima namna ya kuwajibu mawakala wa sense watakapofika majumbani mwao.
Akifafanua kauli hiyo sheikh ponda amesema watakapofika mawakala wa sense wawajibu tumepata maelekezo kutoka kwa viongozi wetu wadini tusihesabiwe hadi mkakubalianenao kwanza baada ya hapo mtatuhesabu.
Aidha Sheikh Ponda alitoa sababu za kutokuwa na imani na Sensa hiyo.
*Sababu ya kwanza ni serikali kutokuwa na mazingira rafiki yanayowezesha sensa ya watu na makazi kuwepo nchini.
*Mfumo wa sensa hauwezeshi madhumuni ya sensa kufikiwa.
*Sensa ili iwe sense nilazima iwahesabu watu wote husika.
* Zoezi lenyewe limegubikwa na matumizi ya mabavu.
Kutokana na hayo taasisi hiyo imetoa msimamo ufuatao, Sensa hiyo inayotarajiwa kufanyika nchini siyo yenye misingi ya haki na ukweli.
Waisilamu chini ya uongozi na mabaraza na jumuiya zisizopungua 30 wamejiandaa kutoshiriki zoezi hilo.
Aidha wameishauri serikali kusitisha zoezi hilo ili kuepusha ufisadi wa pesa za umma na kuweka misingi bora ya zoezi hilo.
Hadi sasa mikoa iliyothibitisha kuandaa maandamano hayo ni Kigoma Tabora Mwanza Arusha Pwani Morogoro na Dar es Salaam yenyewe.
Wamelaani propaganda na matumizi ya nguvu.
Hata hivyo sheikh Ponda alimalizia kwakutangaza kufanya maandamano nchi nzima siku ya Jumatano August 29 mwaka huu.

Mwisho:

Post Top Ad

Responsive Ads Here