Rashid Matumla na
Mtambo wa Gongo, kutwangana siku ya Eidd.
Mabondia Maneno Osward kushoto na Rashidi Matumla wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mpambano wao utakaofanyika siku ya uidi pili katika ukumbi wa Dar live siku ya Idi mosi |
Juma Kassim Nature akiahidi burudani ya aina yake siku hiyo. |
Mwasiti Almasi naye atakuwepo siku hiyo. |
Linna Sanga atatumbuiza pia. |
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA wakongwe nchini, Rashid Matumla 'Snake Man' na Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo', watapigana pambano la kustaafishana siku ya Idd Mosi kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.
MABONDIA wakongwe nchini, Rashid Matumla 'Snake Man' na Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo', watapigana pambano la kustaafishana siku ya Idd Mosi kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.
Pambano hilo limeitwa la
kustaafishana kwa sababu, bondia mmoja atakayepigwa, atatakiwa kustaafu ngumi
kutokana na makubaliano ya pambano hilo.
Mratibu wa burudani wa Dar Live,
Luqman Maloto, aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, Matumla
na Maneno watapigana pambano la raundi 10, kisha litafuatiwa na mambano mengine
mawili na atakayepigwa atastaafu ngumi.
"Mabondia wenyewe ndiyo
walitaka kuwe na pambano la aina hiyo, kwa hiyo mashabiki wao waje kwa wingi
siku ya Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live ili wapate picha ni nani kati ya mabondia
hao anaweza kustaafu.
"Siku hiyo itakuwa ni uzinduzi
mpya wa Ukumbi wa Dar Live, kwa hiyo kutakuwa na shoo kali ya muziki wa kizazi
kipya kutoka kwa wanamuziki wakali, Mwasiti Almasi, Maunda Zorro, Estelina
Sanga 'Linah', Mzee Yusuf akiwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab bila
kumsahau Juma Nature na TMK Wanaume Halisi pia atakuwepo," alisema Maloto.
Kwa upande wa mabondia hao, kila
mmoja ametamba kumchakaza na kumstaafisha mwenzake, wakati wanamuziki hao, nao
wakiahidi kutoa burudani ya nguvu kwa ajili ya siku hiyo ya furaha baada ya
mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kuhusu watoto, Luqman, alisema siku hiyo
watapewa kipaumbele, kwani watapewa chakula kwa ajili ya kusherehekea sikukuu,
vile vile wale watakaokuwa wanasherehekea siku ya kuzaliwa, watafanyiwa sherehe
pale pale.Super
D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake
ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa.