Vurugu zaigubika
Kariakoo, mabomu yalipuliwa, Chanzo mgogoro wa nyumba, mitaa
ya fungwa hadi mida hii.
Nyumba inayo gombaniwa na kuzua tafrani kabla haijaanza kuvunjwa eneo la mtaa wa Kongo Kariakoo.
Mmoja wa majeruhi wa mabomu ya
machozi kwenye vurugu hizo akiondolewa eneo la soko la Kariakoo baada ya
kuunguka chini kutokana na milipuko hiyo, ambayo iliambatana na mawe yalikuwa
yakirushwa na vijana waliokua wakitetea upande mmoja wa ugomvi huo.
Askari wa Kikosi Cha kutuliza Ghasia
FFU wakiweka chini ya ulinzi mkali eneo la Kariakoo baada ya kufunga mitaa ya
Kongo nay a jirani kutokana na kuibuka vurugu zilizotokana na ugonvi wa nyumba
ambayo kwa maelezo ya watu wa karibu nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro kwa zaidi
ya miaka 20 kati ya wamiliki na wapangaji kutokana na kutengeneza hati feki.
Mitaa ya Kituo cha Polisi Msimbazi Kriakoo
ikiwa mitupu bila ya watu wengi kama ilivyozoeleka ni askari tu ndio waliokuwa
wakiranda kwenye eneo hilo.
Mtu ambaye alijitambulisha kwa jina la Samir Sadick, alidai yeye ndie msimamizi wa nyumba hiyo ambayo inamilikiwa na mamayake, ambapo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameipigania hakiyao kwa miaka ishirini hadi leo wanaipata kutokana na kesi waliyofungua mahakamani wakidai kunyang'anywa nyumba yao na wapangaji kwa kutengeneza hati feki.Nyumba inayo gombaniwa na kuzua tafrani kabla haijaanza kuvunjwa eneo la mtaa wa Kongo Kariakoo.
Hapa vijana wa kazi wa kampuni ya
Yono Auction Mart iliyopewa tenda ya kusimamia ubomoaji wa nyumba hiyo chini ya
ulinzi mkali wa pilisi wakiendelea na kazi kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa
Kon
Mashuhuda nao walikuwepo tangu zoezi linaanza na walikuwepo pia wanaoufahamu mgogoro huo na kudai kuwa nyumba hiyo anadhulumiwa mzaramo na Mwarabu kwasababu anapesa, lakini wengine wakasema nyumba hiyo imeuzwa mara tatu tofauti na kuzua mgogoro huo. |
No comments:
Post a Comment