Rais wa Liberia amsimamisha kazi mwanae.
RAIS wa
Liberia Ellen Johnson Sirleaf, amemsimamisha kazi mmoja wa watoto wake wa kiume
kutoka ngazi ya unaibu gavana wa benki kuu ya nchi hiyo kwa kushindwa
kuorodhesha mali zake katika tume ya kuzuia rushwa nchini humo. Charles
Sirleaf, ni miongoni mwa maafisa 46 waliosimamishwa kazi kwa kosa hilo.
Ni mmoja wa watoto wake
watatu wa kiume aliowateua kushika vyeo vya juu kabisa baada ya kushinda muhula
wa pili wa uchaguzi mwaka jana.Wapinzani wa Bi Sirleaf wanamshutumu kwa kuendeleza
upendeleo wa kindugu. Rais huyo amemteua mtoto wake wa kiume Fumba kuwa mkuu
idara ya usalama wa taifa, na kijana mwingine Robert kuwa mshauri mkuu na
mwenyekiti wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali-NOCAL.
Utawala boraRobert Sirleaf
anayashitaki magazeti mawili nchini humo ya Independent na Analyst, na
mwanasiasa wa upinzani Jefferson Kogie kwa kumkashifu kuwa amejinufaisha kifedha
kutokana na vyeo alivyopewa. Taarifa kutoka ofisi ya Bi Sirleaf imesema Charles
Sirleaf na maafisa wengine 45 wataendelea kuwa wamesimamishwa kazi hadi hapo
watakapoorodhesha mali zao kwa Tume ya Kuzuia Rushwa.
Maafisa wengine
waliosimamishwa kazi ni pamoja na mkuu wa itifaki ya rais, David Anderson,
Wakili mkuu na naibu waziri wa sheria Micah Wilkins Wright na naibu mkurugenzi
mkuu wa utangazaji Ledgerhood Rennie.
Liberia
Alitunukiwa tuzo ya amani
ya Nobel mwaka jana, muda mfupi baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine
katika uchaguzi ulioghubikwa na tuhuma za udanganyifu katika zoezi la upigaji
kura. Rushwa bado inabakia kuwa kikwazo kikubwa nchini Liberia huku idadi kubwa
ya watu wakiishi katika umasikini licha ya utajiri mkubwa wa madini nchini
humo.
Rais wa Liberia Bibi Ellen
Johnson Sirleaf.
Bi Sirleaf aliyeingia
madarakani mwaka 2005 mwishoni mwa mgogoro wa vita Uliodumu miaka 14, amekuwa
akiahidi mara kwa mara kupambana na rushwa na kustawisha utawala bora nchini Liberia.
Mwezi Juni taasisi ya
kimataifa ya Maafa-ICG, ilitoa ripoti kutahadharisha kuwa rushwa na upendeleo
wa kindugu katika sekta mbalimbali vinaweza kuhatarisha demokrasia nchini humo.
No comments:
Post a Comment