SENSA YAAMSHA HASIRA ZA WAISILAMU. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, August 20, 2012

SENSA YAAMSHA HASIRA ZA WAISILAMU.

BAKWATA, Yachanwa chanwa viwanja vya  Mwembeyanga, Ni kwenye Baraza la Eid, waislamu wajitokeza kwa wingi wasema hakuna kuhesabiwa mtu. Siku ya sensa waisilamu kukusanyika misikitini kufanya dua maalum kulaani wasaliti.

 Waumini wa dini ya kiislamu waliofurika kwenye viwanja vya mwembe yanga kwenye baraza la Eid, ambalo kwa kiasi kikubwa mada kuu ilikua moja tu ni kupinga zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
 Hapa waisilamu hao wakifuatilia kwa makini hoja zinazotolewa na viongozi wao kwanini wasishiriki kwenye zoezi hilo la kuhesabiwa, ambapo kwaumoja wao waliapa kutoshiriki kwenye zoezi hilo.
 Masheikh Mbalimbali waliohudhuria kwenye Baraza hilo kwenye viwanja vya Mwembe yanga jana jioni
 Aimiri wa Shura ya Maimamu Sheikh Mussa Kundecha (kulia ) akiwa na Sheikh Gumbo (katikati) wakati mawaidha mbalimbali yakitolewa kwenye viwanja hivyo.
 Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akisalimiana na viongozi wa dini hao mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
 Moja ya mabango ya kubandika majumbani mwa wailamu kwaajili ya kuwazuia waandishi wa sensa kutofika kwenye nyumba zao siku ya sensa hiyo.
 Imamu wa Msikiti wa Idrissa Sheikh Ally Basaleh akiwahutubia waumini hao kwenye viwanja hivyo.
 Sheikh Kondo Juma Gumbo, akiwahutubia waumini hao akiwa amepewa mada ya katiba.
Kila mmoja alifuatilia kwa makini mwanzo hadi mwisho na kuamua kuondoka na msimamo wakutohisabiwa baada ya kulishwa kiapo na masheikh hao na atakae geuka msimamo wake atfikwa na majanga.


NI KWENYE mgogoro mzito unaoendelea kati ya Serikali na baadhi ya waumini wa dini ya kiisilamu nchini wanaopinga zoezzi la sensa wakiwa na madai mbalimbali ambayo tayari walisha yawasilisha kwenye kamati inayosimamia zoezi la Sensa. Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na kisiasa na tamko la kupinga sensa lilisomwa na sheikh Ponda Issa Ponda.

Mbali na kutolewa tamko ilipitishwa harambee ya kuchangisha fedha kwaajili ya kuwatumia masheikh waliosambazwa mikoani kwaajili ya kuhamasisha waisilamu wasikubali kuhesabiwa.

Naye Imamu wa Msikiti wa Idrissa Sheikh Ally Basaleh, alisema kitendo cha bakwata ambayo ni taasisi moja tu miongoni mwa taasisi nyingi za waislamu kujifanya wao ndio wanamlaka ya kuwafanyia maamuzi waislamu hakikubaliki hata sikumoja.

“Niupunguvu wa fikra mufti Simba kujidanganya kwamba yeye ndie mwenye mamlaka ya kumteua kadhi, ambapo alisisitiza kuwa waisilamu hakudai kadhi ila wanataka mahakama ya kadhi kama makadhi tu wapo wengi lakini siyo wanaohitajika na waislamu,” alisema Basaleh.  Bakwata imekua ni kikwazo kikubwa kwazo kikubwa kwa harakati za waislamu hao kwani pamoja na wao kushiriki kwenye harakati za mwanzo kabisa kupinga sensa ikiwemo kuibua hoja kadhaa kwnye kadhia hiyo lakini msimamo wao ulidumu kwa sikumbaili tu baadaye  wakaufyata. Miongoni mwa maswali ambayo serikali haina majibu halisi ni kama kweli hoja ya serikali kuwa haina dini hivyo haina haja ya kujua idadi ya watu wenye dini  je kwanini kwenye zoezi hilo wanahesabu misikiti na makanisa? Ili iweje au kwakua wanajua kwamba makanisa ni mengi kuliko misikiti?

Vipeperushi na mabango yakubandika kwenye nyumba za waislamu vimezinduliwa na kuuzwa kwa waumini hao ambapo mawakala wa sensa hawataruhusiwa hata kukaribia kwenye nyumba zenye makaratasi hayo.

Mbali na mabango hayo pia tamko hilo limewataka waisilamu wote siku ya sensa kwenda misikitini kusali sala maalumu ya kuwalaani wote wanasaliti waisilamu kwenye zoezi hilo.
Baraza hilo la Eid ambalo lilihudhuriwa na Mwenyekiti CUF Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Mbunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima na wengine kadhaa.

MWISHO.

Post Top Ad

Responsive Ads Here