Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) amtwanga Rashid
Matumla kwa Points.
Bondia Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) akimtandika makonde ya uso bondia Rashid Matumla kwenye mpambano uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Dar Live, ambapo Osward alishinda kwa Points.
Hpa ngumi zilichangamka kwelikweli kila mmoja akitupa makonde ya uhakika kwa mwenzake lakini mwisho wa siku Mtambo wa Gongo akaibuka kidedea. Mpambano huo ulikua ni mpambano wa kustahafishana kutokana na wapiganji hao kuwa ni mabondia wakongwe nchini wakiwa njiani kuachana na mchezo huo wa masumbwi.