Papaa
Msofe yamemkuta, apandishwa kizimbani kisutu Chini ya
Ulinzi Mkali, Tuhuma ni za mauaji 2011.
Mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam Marijani Abubakari, almaarufu kama papaa msofe (shati la blue) akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi wakati akifikishwa kwenye mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa tuhuma za mauaji. |
Papaa Msofe, akitoa maelezo kwa jeshi la Polisi alipofika kisutu. |
Akiingia kwenye Chumba cha Mahakama.
MFANYABIASHARA maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani
Abubakar, alimaarufu kwa jina la Papaa Msofe leo amefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la tuhuma za mauaji.
Papa Msofe amesomewa shitaka hilo mbele ya hakimu Tumaini Mchome kuhusu mauaji
ya marehemu Chasphori Kituli yaliyofanyika Oktoba 6, 2011 Magomeni Mapipa kwa
kupigwa risasi.
Papa Msofe hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena Agosti 23 mwaka huu.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi Magomeni akituhumiwa
kuhusika na mauaji ya aliyekuwa mfanyabiashara mwenzake, marehemu Kituli.
Marehemu alikuwa akimiliki migodi Mererani, Arusha, na muda mrefu
walikuwa na mgogoro wa kudaiana ambapo inadaiwa marehemu alikuwa anadaiwa na
Papa Msofe Sh. milioni 30.
Habari na Picha kwa Hisani ya Global
Publisher.
MWISHO:
|