Tigo yakabidhi vitabu
300 Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), ni muondelezo wa program
yake ya kurejesha sehemu ya faida kwa jamii.
|
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Ludovick Kinabo (katikati) akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa meneja uhusiano na udhamini wa Tigo Edward Shila,Msaada huu ulikuwa ni muendelezo wa msaada wa vitabu uliotolewa mwaka jana na kampuni hiyo hapo chuoni kwania ya kurudisha sehemu ya faida kwa jamii inayoihudumia, anayeshuhudia ni mkurugenzi wa Tigo kanda ya kati, Fadhila Said. |
|
Meneja uhusiano na udhamini wa Tigo, Edward Shila, akionesha maboksi ambayo ndani yake kuna vitabu 300 vilivyotolewa na kampuni ya Tigo kusaidia maendeleo ya elimu katika chuo cha UDOM. |
|
Makamu mkuu wa chuo cha UDOM, profesa Ludovick Kinabo (katikati) akiishukuru kampuni ya Tigo kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya chuo cha UDOM, kulia ni meneja uhusiano na udhamini wa Tigo, Edward Shila pamoja na mkurugenzi wa Tigo kanda ya kati, Fadhila Said. |