Kufa kwa…… Haja ku……., Familia ya Mafisango yatupiwa vyombo nnje.
Orly Ilemba, akiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu kaka yake, Patrick Mafisango baada ya mwenye nyumba kutoa nje vyombo vya ndani kutokana na deni la pango |
Baadhi ya watoto wa familia hiyo wakiwa hawajui lolote linaloendelea. |
Vyombo vya Mafisango vikiwa nje y nyumba hiyo. |
FAMILIA ya aliyekuwa kiungo mahiri wa
mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba, marehemu Patrick Mutesa Mafisango iko
katika wakati mgumu baada ya kutimuliwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi, Keko
Bora jijini Dar es Salaam.
Familia hiyo, ilitolewa
nje vifaa katika nyumba hiyo na mmiliki wake, kutokana na kudaiwa kodi ya pango
aliyokuwa akiudai kwa muda mrefu
uongozi wa Simba.
Akizungumza kwa masikitiko
makubwa jana, mdogo wa marehemu Mafisango, Orly Ilemba, alisema, mwenye nyumba
huyo, Chingweni Mtoro, aliwafuata asubuhi na kutaka chumba chake kabla ya kutoa vitu hivyo nje ya chumba na kuweka kufuli jipya.
“Nipo nje tokea asubuhi, hatujafanya
lolote, zaidi nalinda vitu vya marehemu, viongozi wa Simba kila nikijaribu
kuwapigia simu hawapokei mpaka sasa sina la kufanya,” alisema Ilemba.
Alifafanua kuwa, viongozi hao wa Simba
walijua mwisho wa kukaa humo, lakini wameshindwa kushughulikia suala hilo
mapema mpaka wanakutwa na aibu hiyo.
“Lakini mwenye nyumba huyu,
alisema mkataba huo ulitakiwa kufika mwisho Agosti 8, kama walivyokubaliana na
viongozi wa Simba, lakini mpaka jana viongozi hao hawakuweza kumalizana naye
ndio maana kaamua kufikia hatua hii,” alisema kwa masikitiko.
Mdogo huyo wa marehemu Mafisango, yupo
nchini kwa ajili ya kusubiria rambirambi, ambazo klabu ya Simba iliahidi
kuzitoa.
Juhudi za kuupata uongozi wa klabu ya
Simba, kujua wana taarifa na wanachukua hatua gani, zilishindwa kuzaa matunda
kwani wahusika, hawakupatikana.
Mafisango kati ya nyota
mahiri waliochangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita iliyofikia
tamati Mei 6, alifariki dunia Mei 17, 2012 kwa ajali ya gari, eneo la Keko,
jijini Dar es Salaam.
Juhudi za kuupata uongozi wa Simba
kuzungumzia hali hiyo ilishindikana baada ya baada ya simu msemaji wa
klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga kutopatikana kwa siku ya jana.
Kwa Hisani ya Super D.
MWISHO: