MIAMBA
ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na
aliyekuwa bingwa
wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni
Jumamosi hii kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila
walitwangana mpambano wao uliofanyika morogoro hata hivyo ulizua utata
baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambalo cheka
aliibuka na ushindi wa point. Akizungumza
Dar es Salaam leo, promota wa pambano hilo Oswald Mlay, alisema pambano
hilo litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba . Alisema
pambano hilo litakuwa la raundi 12 uzito wa kg 72 ambapo leo wamepima
uzito kwa ajili ya mpambano uho utakaoamua nani zaidi
Katika
Mchezo huo kutakua na uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi
pamoja na
kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa
mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili
ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua
sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether,
Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na
wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao
ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa
matano ya utangulizi. |
No comments:
Post a Comment