Waisilamu wacharuka duniani
kote, Katibu Mkuu
wa UN alaani Filamu hiyo. Marekani yakosolewa.
-->MAANDAMANO ya kupinga filamu inayokashifu dini ya kiislamu na mtume wake Muhammad yanaendelea kwenye nchi za kiarabu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani filamu hiyo ambayo ameiita ni ya chuki. Naye mpinzani wa Rais Barack Obama kwenye uchaguzi wa urais
Novemba mwaka huu, Mitt Romney, amekosoa namna serikali ya Marekani
inavyoshughulikia mauwaji ya maafisa wake wa ubalozi.
-->MAANDAMANO ya kupinga filamu inayokashifu dini ya kiislamu na mtume wake Muhammad yanaendelea kwenye nchi za kiarabu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani filamu hiyo ambayo ameiita ni ya chuki.
Zaidi ya waandamanaji 200 wamejeruhiwa katika maandamano
yanayoendelea kwenye ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kupinga
kudhalilishwa kwa Mtume Muhammad kupitia filamu iliyotengenezwa nchini
Marekani. Polisi wamemwagwa kwenye eneo lililo karibu na uwanja wa
Tahrir wakifyatua mabomu ya machozi dhidi ya waandamanaji ambao wanarusha mawe.
Kituo cha televisheni cha taifa kimeinukuu wizara ya afya ikisema kuwa watu 224
na askari 31 wamejeruhiwa katika vurugu hizo. Yasambaa nchi zingine Maeneo mengine ambayo maandamano yameendelea kufanyika ni
pamoja na Libya, Yemen, Lebanon na Iran. Hii leo pia Sudan imetangaza kufanya
maandamano makubwa baada ya sala ya Ijumaa kupinga filamu hiyohiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amelaani
kitendo cha kutengenezwa kwa filamu hiyo aliyoiita ya chuki ambacho
kimesababisha vifo vya balozi wa Marekani nchini Libya, Christopher Stevens,
pamoja na afisa habari wa ubalozi huo, Sean Smith.
Watu wengine wawili waliouawa kwenye mashambulizi hayo
wametambuliwa kuwa ni Tyrone Woods na Glen Doherty, wanajeshi wa zamani wa
vikosi vya majini waliokufa wakijaribu kuwaokoa wenzao. Ban ametoa wito wa kuwepo na utulivu, uvumilivu na
kusisitiza kuwepo mazungumzo ya amani katika kutatua suala hilo. Awali Waziri
wa Mambo ya kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, alilaani pia filamu hiyo na
kusema Marekani haihusiki kwa namna yoyote katika utengenezaji wake.
"Serikali ya Marekani haihusiki hata kidogo na filamu
hiyo. Tunakemea kwa nguvu maudhui na kila kilichomo kwenye filamu hiyo.
Uvumilivu wa Marekani kwenye masuala ya dini uko tangu mwanzoni kabisa wa taifa
letu na kama unavyojua sisi ni nchi ya watu wa dini zote" ,alisema Bbibi
Clinton.
Kauli ya Romney
Kitendo cha Rais Barack Obama na Clinton kulaani filamu hiyo
kimemkasirisha Mitt Romney ambaye ameukosoa utawala wa Marekani kwa namna
unavyoshughulikia suala hilo. Akiwa kwenye kampeni zake Virginia kaskazini,
Romney amesema kuwa sasa inaonekana kuwa mhurumiaji wa dunia na kutaka kuwepo
kwa jeshi imara zaidi la nchi hiyo. Amemtuhumu Obama kuwa anawaomba radhi
maadui wa Marekani badala ya kulaani mauwaji.
Hata hivyo kauli hiyo ya Romney imepata upinzani sio tu
kutoka kwa wafuasi wa chama cha Democratic bali pia wenziwe wa chama cha
Republican. Wachambuzi wanasema kuwa Romney alikurupuka kutoa kauli kama hizo
katika wakati usiofaa kwani Obama na Clinton wote wamelaani mauwaji hayo. Rais Obama mwenyewe amesema kuwa Romney ni mzuri
wakukimbilia kufyetua risasi na kisha baadaye kulenga shabaha na kuongeza kuwa
mtu wa aina hiyo hafai kuwa rais wa taifa kama Marekani.
No comments:
Post a Comment