KUFUATIA MAANDAMANO YA WAISILAMU YANAYOENDELEA - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, September 15, 2012

KUFUATIA MAANDAMANO YA WAISILAMU YANAYOENDELEA

Mataifa ya magharibi yatoa wito kusitishwa maandamano.

 An Egyptian protester runs with a tear gas canister to throw it back at riot police during clashes near the U.S. embassy in Cairo.
 An Indian protester kicks at an image of the American flag on a wall of the U.S. Consulate during a protest against the anti-Islam film which depicts the Prophet Muhammad as a fraud, a womanizer and a madman, in Chennai, India.
 A boy holds a toy gun during a protest against the film "Innocence of Muslims", in the Palestinian refugee camp of Ain el-Hilweh near Sidon, Lebanon, on September 14, 2012. (AP Photo)
 Bangladeshi Muslims attempt to break a police barricade during a protest in Dhaka, Bangladesh, on September 14, 2012. Around 10,000 Muslims from half a dozen Islamist groups staged a noisy protest in the Bangladesh capital Dhaka on Friday over the U.S. film said to have insulted the Prophet Mohammad. (Photo/Reuters)

MATAIFA ya nchi za magharibi yametaka kukomeshwa kwa maandamano yenye lengo ya kushambulia balozi za nchi hizo kupinga filamu inayomdhalilisha mtume Muhammad iliyotengenezwa nchini Marekani.
Jumuiya ya Ulaya imewataka viongozi wa nchi za Kiarabu na nchi nyingine za kiislamu kuacha maandamano na kudumisha amani. Marekani inatuma wanajeshi wake kulinda ubalozi wake ulioko Khartoum nchini Sudan ikiiasa pia Sudan kulinda balozi za kigeni nchini humo.
Watu wasiopungua saba waliuawa katika maandamano ya ghasia mjini Khartoum, Tunis na Cairo siku ya Ijumaa, na kuna wasiwasi wa kutokea maandamano zaidi. Wanajeshi wa Marekani walipelekwa pia nchini Libya siku ya Jumatano baada ya balozi wa Marekani nchini Libya na Wamarekani wengine watatu kuuawa pia nchini Yemen siku ya Ijumaa baada ya ghasia za maandamano mjini Sanaa.
Nchini Afghanistan, wapiganaji wa Taliban wamesema pia wameshambulia moja ya kambi kubwa za vikosi vya kimataifa nchini humo ya Bastion ambapo wanajeshi wawili wa Marekani waliuawa. Wapiganaji hao wanadai kufanya shambulio hilo kulipiza kisasi kupinga filamu hiyo ya kuukashifu uislamu.
Waandamanaji wakipinga filamu hiyo mjini Sydney Australia siku ya Jumamosi, 15 Septemba 2012 Waandamanaji wakipinga filamu hiyo mjini Sydney Australia siku ya Jumamosi, 15 Septemba 2012
Balozi za Ujerumani na Uingereza nchini Sudan pia zilishambuliwa ingawaje uhusiano juu ya filamu hiyo na nchi hizo haujafahamika. Siku ya Ijumaa rais wa Marekani Barack Obama na Waziri wa mambo ya nchi za nje Hillary Clinton walihudhuria mapokezi ya kurejeshwa Wamarekani waliouawa mjini Benghazi nchini Libya.

Bwana Obama alisema kuwa Marekani itakabiliana vilivyo dhidi ya mashambulizi yoyote kwa balozi zake nchi za nje. Maandamano zaidi yameripotiwa kuenea zaidi hadi nchini Australia ambapo polisi walipambana na mamia ya waislamu katika mitaa ya jiji la Sydney.

Polisi hao walitumia gesi ya kutoa machozi na mbwa kujaribu kuwasambaratisha waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe na miti.
 Mtengenezaji ahojiwa
Wakati huohuo mmoja wa watu wanaoshukiwa kuhusika na utengenezaji wa filamu hiyo inayolalamikiwa kuukashifu Uislamu, amehojiwa na maafisa wa polisi mjini Los Angels nchini Marekani.
Wanataka kujua iwapo alikiuka masharti ya msamaha wa parole aliokuwa amepewa kufuatia adhabu ya kifungo kwa makosa ya kughushi. Aliadhibiwa adhabu ya kifungo jela mwaka 2010 kwa kughushi kujipatia fedha benki na baadaye alipewa msamaha wa masharti.
Adhabu hiyo pia ilimpiga marufuku kutumia vifaa vya kompyuta na intaneti.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here