Waziri mkuu wa
Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, apata jiko.
Waziri Mkuu wa Zimbabwe akiwa na Mkewake Elizabeth Macheka mara baada ya kufunga ndoa siku ya jumamosi jana.
WAZIRI mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amefunga ndoa
siku ya Jumamosi licha ya hukumu ya mahakama kutoa hukumu ya inayozuia ndoa
hiyo kufanyika.
Siku ya Ijumaa mahakama ilifutilia mbali leseni ya ndoa ya
Bwana Tsvangirai ikisema kuwa tayari anatambulika kuwa ameoa mwanamke mwingine
katika sheria za kimila.
Mwandishi wa BBC nchini Zimbabwe anasema kuwa baadhi ya
wafuasi wa Bwana Tsvangirai wanaamini kuwa hukumu hiyo ya mahakama imepikwa
kisiasa ili kumchafulia jina Waziri mkuu huyo kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment